Prof Kitila Mkumbo Aanza Kazi kwa Kuishushia Mkwara Mzito Dawasco..!!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Katibu mkuu wa wizara ya maji Prof: Kitila Mkumbo amelitaka shirika la maji safi na taka nchini DAWASCO kuhakikisha wanawekeza sana kwenye usambazaji wa maji kwani ni aibu kwa jiji la Dar es salaam kuwa na maeneo ambayo hayana maji.

Prof: Kitila Mkumbo ametoa maagizo hayo jana jijini Dar es salaam wakati alipofanya ziara katika shirika hilo na kukutana na watendaji wakuu wa DAWASCO pamoja na watendaji wakuu kutoka Mamlaka ya maji safi na taka jijini Dar es salaam DAWASA.

“Pamoja na kazi nzuri mnayofanya ya kuhakikisha upatikanaji wa maji hakikisheni mnaongeza kasi ya usambazaji wa huduma hii muhimu kwa wananchi kwa kufanya hivyo mtakuwa mnatendea haki dhana ya kuwa mnaongoza kwa mapato lakini pia mnatoa huduma stahiki kwa wananchi”. Alisema Prof. Kitila

 Pamoja na hayo amewasii wateja wote wa DAWASCO kutii agizo la Mhe. Rais kwa kulipia huduma wanazozipatiwa ili kuziwesha mamlaka hizo kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Prof: Mkumbo pia amelitaka shirika hilo kukamilisha miradi ya maji katika maeneo ambayo mpaka sasa inaonekana haijakamilika kwa lengo la wananchi kupata maji.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad