Usipuuzie..Mara Uonapo Dalili Hizi 8 Wahi Haraka Hospitali ..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Kuna wakati unaweza kujikuta hauko vizuri kila siku na ukashindwa kujua nini tatizo.

Sasa leo napenda tujuzane hizi dalili ambazo ikiwa utaziona basi huenda ukawa na matatizo kiafya:-


1. Kupungua uzito ghafla.
Kuna baadhi ya watu huweza kujikuta ghafla tu wamepoteza kilo kadhaa bila kuwepo na sababu za msingi, hivyo wataalam wa afya wanashauri inapotokea hali hiyo ni vyema kufanya uchunguzi zaidi ili kubaini sababu za msingi za hali hiyo kutokea.

2. Mabadiliko ya ngozi.
Ngozi ni alama tosha ambayo huashiria uwepo wa afya bora kwa binadamu hivyo basi ikiwa utaona ngozi yako imeanza kupoteza uhalisia wake basi ujue huenda tayari kunatatizo la kiafya linakunyemelea hivyo unaweza kuwaona wataalam kwa ushauri zaidi.

3. Mabadiliko ya haja ndogo
Unapoona kuanza mabadiliko ya haja ndogo au haja kubwa basi huenda nayo ikawa dalili ya tatizo, hivyo ni vyema kuwa mchunguzaji wa haja zako ili kung'amua baadhi ya matatizo ya kiafya kwa haraka na kuyatafutia ufumbuzi kwa wataalam.

4. Matatizo ya kukosa usingizi.
Hii nayo huweza kuwa ni kiashiria cha tatizo mwilini mwako hivyo unapoona mabadiliko yanahusu usingizi pia unaweza kujichunguza vizuri na unapoona huelewi basi waone wataalam kwa ufafanuzi zaidi.

5. Midomo kukauka.
Unapoona midomo inakauka au kupasuka nayo huweza kuwa dalili mbaya kiafya hivyo unaweza kufanya maamuzi ya kwenda kufanya uchunguzi wa kiafya ili kujua tatizo zaidi.

6. Mabadiliko ya joto la mwili
Iwapo mwili unakuwa na joto mara kwa mara nayo huweza kuwa ni moja ya kiashiria cha tatizo kiafya, hivyo ni vyema kuwaona wataalam kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa kiafya.

7. Unapokosa hamu ya kula kabisa
Nayo ni moja ya dalili kuwa mwili wako unashida hivyo ni muhimu kufika kwenye kituo cha afya kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

8. Uchovu wa mwili
Mwili unapojihisi umekuwa mzito nayo huwa dalili ya tatizo ndani ya mwili wako nayo si vizuri kuipuuza na badala yake ni vyema kufanya uchunguzi zaidi.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad