Mke Wangu Kalipenda Hili Jitu Nini?

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Waheshimiwa nina mgeni ambae sasa anaelekea kumaliza wiki akiwa hapa kwangu, ni binamu yangu huwa anaishi mkoani amekuja kwa shughuli zake binafsi, ataondoka atapokamilisha yaliyomleta.

Nimewaandikia kwa sababu, huyu jamaa amenishangaza sana, imagine weekend hii iliyokwisha anashinda na boxer kutwa nzima tena kifua wazi, au kwasababu amevimba kifua anataka tumwone au?

Mke wangu na house girl wanafua nguo Jumamosi asubuhi eti anaenda pale awasaidie kufua, natoka ndani namuuliza wife mbona mgeni anafua nguo, najibiwa kuwa eti ameomba mwenyewe, hii ni sawa kweli?

Yote tisa, kumi ni Jana, inafikia hatua linamkuta wife jikoni anasonga ugali linaomba limsaidie kusonga ugali, mgeni gani wa namna hii?

Wadau nitumie njia gani kulitimua hili jitu hapo nyumbani? Kabla halijaleta madhara maana mdogo wa mke wangu naona kama yuko nalo karibu sana, pia wife kaniuliza kama mimi pia naweza kufanya mazoezi nikawa kama hilo jitu badala ya kitambi, ingawa alinieleza kwa utani huku tukifurahi na kutaniana ila najiuliza kwanini aseme sasa wakati hili jitu lipo?

Linakaa hapo sebuleni kwenye video hadi usiku mwingi likiwa na mdogo wa mke wangu bila kujali maadili.

Jumapili nilienda kwenye Bonanza la timu yetu ya veterans narudi nimekuta nyumba nzima hawapo wameenda beach wote pamoja na huyu jamaa.

Hivi unaendaje ugenini halafu unaanza kuleta ujuaji wa namna hii?

Wadau msaada wa mawazo unatakiwa haraka.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. mchane live mwambie sipendi utoke na familia yangu wala kushirikiana nao kazi za home hii tabia siipendi stay within yr limit usimfiche hata kama ni kaka yako tumbo moja mpe live kama shemeji yako kampenda basi waozeshe amuoe

    ReplyDelete

Top Post Ad