AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kanda ya kati kimeitaka serikali kuwalipa fidia wakazi wa Manispaa ya Dodoma ambao kwa namna moja au nyingine wameathirika wakati Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) ilipokuwa ikifanya kazi kwa kuporwa ardhi yao.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Mafunzo na Oganaizesheni wa Chadema, Benson Kigaila wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini hapa.
Kigaila amesema kuwa Rais John Magufuli hawezi kuivunja CDA na ikawa ndiyo mwisho wake bila kuangalia madhara yaliyosababishwa na mamlaka hiyo kwa wananchi katika kipindi chote cha miaka 44 iliyofanya kazi.
Amesema fidia hiyo ni lazima ilipwe na serikali kuu ambayo ndiyo iliyoiweka CDA madarakani na siyo kuliachia jukumu hilo Manispaa ya Dodoma kwa kuwa haihusiki na unyang’anyi huo.
"Kuivunja CDA siyo hoja. Hoja inayokuja hapo ni je wananchi wa Dodoma walionyang'anywa ardhi yao na CDA bila kulipwa fidia watafidiwaje au ndiyo wataachwa waendelee na maumivu yao?" amesema Kigaila
Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu
Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:
NAFASI ZA AJIRA
JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA
GOODLUCK
hapo umenena hiawezekani CDA imeunduwa miaka hiyo ya nyuma na huwezi kukurupuka mara moja uivunje CDA wakati viwanja vya watu walionyanganywa bado hawajalipwa huo ni kama kudhulumu watu jamani tunaenda wapi iko wapi tanzania yetu haya wewe bwana kama umeaumua kufanya hivo usisahau kuwa kina asie lala anaona kila kitu na kujua nia yako kabla hujaamua kutendea tumekuachikia mungu
ReplyDelete