Dk Shein Alivyowajibu Waliosusia Fomu CCM

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Dk Ali Mohamed Shein amewaambia vijana na makada  waliosusia kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho kuwa, ni aibu kutoa kauli ya namna hiyo kwa nchi yao.

Kauli hiyo ya Dk Shein imefuatia ile ya Katibu wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja, Sauda Mbamba aliyesoma taarifa ya mkoa huo mbele ya Dk Shein katika hafla maalumu ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa vijana wa Jimbo la Uzini akisema vijana wengi hawachukui fomu hizo.

Ikiwa ni kama majibu kwa vijana hao, Dk Shein amesema suala la msingi ni kuwa na uzalendo ambao ndiyo mwongozo sahihi katika kulinda heshima na nidhamu ya mtu kwenye jamii na Taifa kwa ujumla.

“Kilio kikubwa cha vijana hao inawezekana ikawa ni suala la ajira, lakini suala hilo ni gumu kwani haiwezekani kila mtu kuajiriwa na Serikali kama wengi wanavyotaka,” amesema.

Makamu huyo wa mwenyekiti wa CCM amesisitiza ajira ni changamoto kubwa kutokana na kuwa kwa sasa idadi ya watu visiwani humo ni kubwa hali inayosababishwa na Wazanzibari kuzaliana kwa wingi ikilinganishwa na nchi nyingine.

“Hivi sasa Zanzibar tumeongezeka sana na hili linachangiwa na sisi wenyewe kwa kuzaa sana, hivyo ni vigumu kila mmoja kupata ajira serikalini kwa kuwa utaratibu wa ajira hauko hivyo,” amesema.

Awali, Sauda alimwambia Dk Dhein kuwa pamoja na chama kutangaza uchukuaji wa fomu za uongozi, bado zimedoda matawini jambo linalohitaji nguvu ya pamoja ya viongozi wakuu kuwashawishi ili wazichukue.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad