IGP Sirro Atangaza Vita Pwani..Adai Ubaya Wataulipa kwa Ubaya..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


IGP Simon Sirro amewaonya wahalifu wanaojishughulisha na mauaji mkoani Pwani kuacha mara moja kwani ndani ya muda mfupi ataenda kuwafichua kwa kutumia vyombo vyake vya dola ili kulinda amani ambayo imepotezwa na kikundi cha watu wachache.

IGP Siro ametoa onyo hilo wakati akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es salaam na kusema kuwa haki lazima iende kutoa majibu ya watu wanaofanya mauaji maeneo ya  kibiti, mkuranga, Ikwiriri kwa ndani ya muda mfupi huku akiongeza hakuna sababu ya watu wema kufanyiwa ubaya na kama jeshi ni wajibu kuilinda amani.

"Hakuna haja ya watu kufanya ukatili na ubaya kwa watu wasiostahili. Sisi tutawajibu ubaya wanaofanya ubaya. Watanzania pamoja na vuiongozi wangu wanataka maji ya nani anayefanya haya mauaji, lakini tayari tumeshapata kujua ni kikundi cha watu wachache niwahakikishie mimi pamoja na vyombo vya dola tutawapatia majibu ndani ya muda mfupi"- IGP Sirro aliwaambia wanahabari.

Pamoja na hayo katika mkutano huo na wanahabari IGP Sirro amewataka wafanyabiashara wa dawa za kulevya kuachana na biashara hiyo haramu kwani hailipi kama jinsi wanavyofikiria na badala yake itawahamisha uraiani na kuwatenga na familia zao kutokana na jinsi watakavyo shughulikiwa na sheria za nchi.

Sambamba na hayo Sirro ametumia nafasi hiyo kuwaasa wananchi kuacha kujichukulia sheria mikononi kwa makosa madogo madogo yanayojitokeza mitaani na kwamba ni kinyume cha sheria za nchi nawote wanaofanya hivyo ameahidi kuwashughulikia kwa sheria.

"Kila mtu atahukumiwa kwa mujibu wa sheria za nchi. Kuna wale watu wanajidai kwamba wanahasira kali hadi kufikia kumuua mtu aliyeiba kuku, niwaambie tu kuku hana thamani ya mwanadamu na hao wenye hasira kali nitaenda nao sambamba kwa sababu imefika hatua eti vifo vya silaha ni vichache kuliko vya hasira kali" - aliongeza IGP Sirro
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad