Rais Magufuli Naye Ametoa ya Moyoni Kuhusu Kifo cha Ndesamburo...!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameeleza kusikitishwa na taarifa za kifo cha Mbunge mstaafu wa Jimbo la Moshi mjini Mzee Philemon Ndesamburo kilichotokea asubuhi ya leo.

Katika salamu za rambirambi alizozitoa Rais Magufuli kwenda kwa wafiwa pamoja na viongozi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amesema amepokea taarifa hizo kwa masikitiko makubwa.

“Kwa masikitiko nimepokea taarifa za kifo cha Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Moshi Mjini, Mzee wangu Philemon Ndesamburo kilichotokea leo tarehe 31 Mei, 2017 katika hospitali ya rufaa ya KCMC iliyoko Moshi Mkoani Kilimanjaro. Namkumbuka Mzee Ndesamburo kwa hekima zake na uongozi wake uliozingatia siasa za kistaarabu” alisema Rais Magufuli

Aidha, Rais Magufuli amesema alifanya kazi na marehemu Philemon Ndesamburo wakati wote wakiwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wakati wote walishirikiana, kutaniana huku akimkumbuka kwa namna ambavyo alitumia muda wake bungeni kupigania mambo yenye maslahi kwa wananchi wa jimbo lake la Moshi Mjini.

Pamoja na hayo, Dkt. Magufuli ameitaka familia ya marehemu Philemon Ndesamburo na wote waliguswa na msiba huo kuwa na moyo wa subira, uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu walichonacho.

Kwa upande mwingine Rais Mgufuli amemuombea dua marehemu apumzishwe mahali pepa peponi
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad