Wakenya kujipima wenyewe Virusi vya Ukimwi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Kenya imezindua kifaa cha bei nafuu cha kujipimia virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Ukimwi, ambacho raia wataweza kukitumia bila usaidizi wa daktari. 

Ili kujipima, mtu anatoa mate, damu au majimaji kutoka mwilini na kisha anajipima binafsi bila ya kusaidiwa na mtu. 

Kifaa hicho kinalenga watu 400,000 ambao hawajafahamu iwapo wana Virusi Vinavyosababisha Ukimwi au la. 

Wataalamu wanasema kwamba, kifaa hicho kinafanikiwa asilimia 80, na kitagharimu kama dola 7 hivi na kitapatikana katika maduka ya kuuzia madawa. 

Martin Sirengo, kiongozi mkuu wa shirika la kukabiliana na Ukimwi Kenya, Nascop, anasema kuwa bado watu watahitajika kwenda hadi katika vituo vya matibabu ili kuthibitisha matokeo. 

Aidha anashauri kuwa, mtu anafaa kujipimia katika sehemu za faragha na mbele ya mtu anayeaminika. 

Rudolf Eggers, mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Kenya, anasema kwamba, “lengo kuu la kifaa hicho cha kujipimia virusi vya HIV ni sambamba na njia nyingine zilizopo za kupima HIV.” 

Takriban watu milioni 1.5 wanaishi na virusi vya HIV nchini Kenya, ambapo milioni moja kati yao wanatumia matibabu ya kumeza vidonge vya kupunguza makali ya ugonjwa wa Ukimwi.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad