Sumaye Nchi Inaendeshwa Kishabiki

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

WAZIRI Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Fredrick Sumaye, amesema nchi inashindwa kuendelea kwa sababu inaendeshwa kishabiki  na kwamba mambo yanayofanyika hayana masirahi kwa taifa.

FREDRICK SUMAYE.
Akizungumza kwenye  Kongamano la Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha) na Umoja wa Vijana wa Vyuo Vikuu ambao ni wanachama wa Chadema (Chaso) jijini Mbeya alipokuwa mgeni rasmi, Sumaye alisema mambo mengi yenye masirahi ya taifa yakifanywa kimzaha yatasababisha madhara kwa taifa.

Sumaye ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, alisema miongoni mwa mambo ambayo ni ya maslahi ya taifa lakini  yanendeshwa kishabiki ni mikataba ya madini na bajeti isiyokuwa na uhalisia.

Mengine aliyoyataja ni uendeshaji wa Bunge ambalo kikatiba ni chombo huru ambacho hakipaswi kuiingiliwa na wabunge kufanya maamuzi kwa maslahi ya vyama vyao vya siasa huku wengine wakishangilia na kuzomeana.

Nchi kwa sasa inayumba na inashindwa kuendelea kutokana na kuendeshwa kishabiki, Bajeti yetu ya mwaka uliopita fedha za miradi ya maendeleo zilitolewa kwa asilimia 34 pekee na serikali ilikiri, lakini sasa hivi wanakuja na bajeti kubwa zaidi ya hiyo ambayo haijatekelezwa na wabunge wa CCM wanashangilia,” alisema Semaye na kuongeza:

Mambo haya yanaliingiza taifa kwenye matatizo makubwa, deni la Taifa linazidi kuongezeka, mikataba ya madini na mingine iliyokuwa ni yenye maslahi ya taifa sasa inakuwa ni ya hasara kwetu, lakini ukiangalia wabunge wanapiga meza wakishangilia.”

Sumaye alisema wasomi wa vyuo vikuu hawatumiki ipasavyo kwa maslahi ya taifa ikiwamo kujadili mikataba na bajeti ya taifa na mawazo yao kutumika katika kufanya marekebisho.

Alisema kipindi hiki ambacho bajeti ya 2017/18 inaanza kujadiliwa leo bungeni, ilitakiwa midahalo mbalimbali ifanyike vyuoni kuichambua, lakini kwa sasa ukifanya hivyo unaonekana umetumwa na vyama vya upinzani, kitu ambacho siyo sahihi.

Alisema miaka ya nyuma viongozi wa serikali walikuwa wanahudhuria katika Ukumbi wa Nkrumah katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kusikiliza mawazo ya wasomi, lakini kwa sasa vyuo vikuu vinatumika kama sehemu ya vijana kupata taaluma pekee.

Alisema Chadema imeamua kujitoa ili kupambana na taabu wanazopata wananchi kwa kuondoa ushabiki wa kisiasa.

Chadema tumeamua kuhakikisha tunawaeleza wananchi ukweli hata kama siasa zimezuiliwa, lakini tutafanya siasa mpya za kutumia akili kubwa,” alisema Sumaye.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. we mzee umetumwa ,hasa upinzani sasa hawana hoja yyt kila kitu kipo kwenye ufanisi kiumakini ktk serikali hii ya hapa kazi.,matusi BUNGENI mtazamwe tu nyie akina nani kisa ubaguzi,kuhusu mikatatba ni hizo serikali zilizo pita na si hii ya ya HAPA KAZI si mnaona madudu ktk sekta ya madini..mzee kayavalia njyga sio km waliopita kuoneana haibu na kufichiana na kufadhiliana...serikali hicho kitu-NO...NB.nyinyi wapinzani LEMA,LISSU nk.ndo mnaleta ushabiki kwa maslahi yenu binafsi..WHY,WHY nyinyi tu kila kukicha..oh SERIKALI MSIWASHITAKI ACCACIA???!!! Onasasa kumbe hawajasajiliwa..BIG UP RAIS WETU J.P.MAGU n GOD will bless u BABA..

    ReplyDelete
  2. Mzee unaongea ushuzi wewe ulikuwa wapi shetani yaani wewe subiri utakufa kama mbwa sasa hivi gpd yetu inapanda viva Magufuli

    ReplyDelete
  3. Hivi si alikuwa PM huyu? alifanya nini zuri kwa nchi hii zaidi ya ulevi? na si ndie aliekuwa akiitwa ZIRO huyu? leo amekuwa nabii wa kukosoa. Haya si ya Mussa ni ya Firauni sasa.kupinga kila kitu.

    ReplyDelete

Top Post Ad