ANNA Mghwira Amng'oa Kiongozi ACT Wazalendo Baada ya Kuteuliwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Ikiwa ni Siku chache baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Act-Wazalendo Anna Mghwira kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkao wa Kilimanjaro leo ameibuka Katibu wa chama hicho Mkoa wa Mbeya  Bahati Longopa na kutangaza kujiuzuluzu nafasi hiyo kwa alichodai kutoridhia uteuzi huo

Longopa amesema  kuendelea kuwa kiongozi wa chama kutampa wakati mgumu kuhamasisha wanachama wapya katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2020.
Amesema kuwa kwa hiari yake ameacha nafasi hiyo ndani ya chama kutokana na kitendo cha viongozi wa juu wa Chama hicho kuingia ndani ya Seriklai iliyopo madarakani ambayo ni ya chama pinzania kwao wao viongozi wa chini hawataweza kuwashawishi wanachama wapya kujiunga na chama hicho
Kuhusu kujiunga na chama  kingine cha siasa amesema kwa sasa ni mapema mno kuzungumzia hilo kwani ataendelea kukaa pembeni na kutojihususisha kwenye mambo ya siasa  huku akitafakari nini cha kufanya.
Mwenyekiti wa ACT- Wazalendo, Wilaya ya Mbeya, Ally Mbika alisema wamepata taarifa  za chini chini, lakini kama chama bado hawajakabidhiwa barua yoyote kutoka kwa kada huyo kutamka kujiuzulu rasmi. 
Amesema  wanasubiri  kukabidhiwa  rasmi ili kuweza kulizungumzia kwa vyombo vya habari barua na  viongozi wa chama  watapitia katiba yao na kupata mwongozo na kuangalia namna ya  kuziba nafasi hiyo mpaka Uchaguzi  Mkuu  wa  mwaka 2020. 
Mbika amesema kuwa kujiengua kwa kada huyo ni pigo kwa chama kwani alikuwa ana mchango mkubwa wa ushawishi na kujenga umoja na mshikamano wa kweli wa ndani na nje ya mkoa.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hii inashangaza. Inamaana Mama Mgwira anaitikadi mbili za Chama? Anakadi ya CCM na ACT Wazalendo na Mamlaka kote? Sijawahi kuiona siasa ya namna hii popote Duniani.

    ReplyDelete

Top Post Ad