KIAMA cha Wahusika wa Mauaji Kibiti Chaja

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

SERIKALI imeahidi kuongeza kasi katika zoezi la ukamataji wa wahusika wa matukio ya mauaji yaliyotokea Kibiti,Rufiji na Mkuranga mkoani Pwani na kuhakiksha wanafikishwa mbele ya vyombo vya sharia.

Waziri Mkuu wa Tanzania ,Kassim Majaliwa aliyasema hayo jana katika baraza la Idd lililofanyika kitaifa katika mji wa Moshi mkoani Kilimanjaro lkitanguliwa na Swala ya Idd El Fitri iliyofanyika kitaifa katika msikiti wa Riadha.

“Kinachofanyika sasa nikuhakikisha kwanza tunawapata waharifu halisi ilikuepuka kuingiza watu wasio husika, kama vile hao wenye hisia kwamba mauaji haya yanafanywa labda na waislamu hapana .”alisema Mh Majaliwa .

Alisema kaz kubwa inayofanywa sasa ni kuchuja na kujua nani hasa anashiriki katika mauaji hayo huku akiwashukuru watanzania ambao tayari wameanza kutoa ushirikiano kwa kuanza kueleza nani wanahusika katika tukio hilo.

“Kazi yetu ni kuwapeleleza pale ambapo tunauthibitisho wa ushiriki wao na hatua kali zitachukuliwa dhidi yao na kazi hiyo inaendelea vizuri.”alisema Majaliwa.

Mapema katika taarifa ya Baraza kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) iliyosomwa na kaimu katibu Mkuu,Sheakh Salim Amir Abeid alisema Bakwata imeshtushwa na matukio ya mauaji ya kutisha ya watu wasio na hatia katika maeneo ya mkoa wa Pwani.

Alisema kutokana na matukio hayo Baraza kuu linatoa pole kwa familia zilizopoteza ndugu na jamaa zao katika matukio hayo aliyoyataja kutokuwa na hata chembe ya kibinadamu .

“Kumekuwepo na matukio ya kutisha ya mauaji ya watu wasio na hatia katika maeneo ya mkoa wa Pwani,matukio ambayo yametushtua sana na kuisikitisha mioyo yetu,baraza kuu la waislamu la Tanzania kwanza kabisa linatoa pole kwa familia zilizopoteza ndugu na jamaa zao katika matukio hayo ya kinyama yasio na chembe ya kibinadamu hata kidogo.”alisema Abeid

Alisema Bakwata inasikitishwa na vitendo vyenye viashiria vya kutaka kuichafua dhima nzuri ya Tanzania kuwa ni kisiwa cha amani na utulivu hasa pale matukio hayo yanapo husishwa na na Dini ya Kiislamu.

“Uislamu ni dini ya amani upendo kuvumilia na nakuishi pamoja na watu wa imani tofauti na kwamba yeyote afanyae matendo yoyote na kinyama kama hayo katu haiwakilishi uislamu na baraza linawataka waislamu kushikamana.”alisema Abeid.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad