Lowassa Afunguka Mazito Kwenye Msiba wa Ndesamburo..Agusia Sakata la Polisi Kuinyanyasa Chadema..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa kamati kuu CHADEMA, Mh. Edward Lowassa amempongeza muasisi wa Chama hicho Mzee Mtei kwa kukutana na Mzee Ndesamburo na kutengeneza chama imara, huku akitoa ahadi ya chama hicho kuongoza mwaka 2020.

Akizungumzaa kwenye ibada ya kuuaga mwili wa Mzee Ndesamburo, Mh. Lowassa amesema kwamba  waasisi hao wameacha  chama chenye nguvu sana na ambacho kinafanya nzuri na kwa weledi.

"Nakupongeza Mzee Mtei kwa kukutana na Ndsamburo. Nakupongeza wewe zaidi kwa sababu umetuachia chama chenye nguvu. Pale nilikuwa namnong'oneza Mzee Mtei kwamba mwaka 2020 tutachukua ushindi,pamoja na jitihada zao mungu atatuongoza na tutaweza" - Mh. Edward Lowassa.

Akizungumzia kuhusu suala la polisi kuzuia eneo la uwanja wa Mashujaa kutumika kumuaga Mzee Ndesamburo, Mh Lowassa amefunguka kuwafariji wafiwa, wanachama na wananchi kwa kuwataka wasamehe yaliyotokea.

"Wamewakatalia uwanja wa Mashujaa lakini hapa kwenye uwanja wa majengo ndo pamega zaidi.Tuwasamehe bure au tuwaachie maneno ya biblia kwamba , Waacheni wafu wazike wafu wao maana hupimi watu kwa uwanja kujaa bali kwa mioyo yao na waliopo hapa ni wale waliompenda na kumuheshimu Mzee wetu" - Mh. Lowassa alifunguka. 
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad