Mbunge wa CCM Ataka Bunge Lipitishe Sheria ya Kuwapima Wabunge Matumizi ya Madawa ya Kulevya..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ally Keissy amependekea kuwapo na sheria ya kuwapima wabunge matumizi ya dawa za kulevya ili kuepukana na ukorofi unaojitokeza bungeni mara kwa mara.

Keissy amesema hayo jana bungeni mjini Dodoma na kusisitiza kuwa yeye atakuwa mstari wa mble kwenye upimaji na endapo itatokea mbunge yoyote yule atakayebisha kupimwa kipimo hicho basi apimwe kwa nguvu na afukuzwe ubunge. 

"Tutengeneze sheria sisi sote hapa tupimwe, inawezekana kuna watu wanatumia madawa ya kulevya humu, tena mimi nitakuwa wa kwanza, tupimwe kuondoa tatizo kwenye bunge letu hili la ukorofi na atakayekataa apimwe kwa nguvu na afukuzwe ubunge haiwezekani kurudia makosa mtu mmoja kila siku anasemwa anarudia yale yale" - alisema Keissy.

Aidha, Mbunge huyo aliendelea kwa kusema kuwa "Adhabu ndogo hii lazima ziwe kali wasipate chochote, wasionekane bungeni muda wa miezi sita au saba ndiyo watashika nidhamu katika bunge hili. Haiwezekani tunaonekana kama tupo Manzese, wabunge wa mjini wamezoea kwenye vijiwe sisi wabunge wa bara hatutaki mchezo mchezo namna hii ya kutukana. Spika kwanza anawazidi umri pamoja na cheo" aliongezea Keissy.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad