Ndugai Ajibu Hoja ya Bunge Kuitwa "Dhaifu"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Spika wa Bunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai amefunguka kuwa wabunge wanaodai kuwa bunge ni dhaifu basi ni wazi watakuwa na mambo yanawasumbua ndio maana wanatoa kauli za kudhihaki chombo hicho.

Mhe. Ndugai amesema hayo leo mjini Dodoma baada ya kuwepo kwa baadhi ya wabunge wanaotoa kauli zisizokuwa rasmi katika vikao vya bunge bila kufikiria kwamba wanachokifanya hakina taswira nzuri kwa wapiga kura wao pamoja na kwa serikali kwa ujumla.

"Yupo mwenzetu alisimama hapa na kulalamika kuwa bunge hili ni dhaifu, kwa maoni yangu hizi ni lugha za kuudhi kwa sababu wenzako wengi namna hii waliochaguliwa na watu wakaletwa hapa halafu wewe unawaona kwa wingi wao ni dhaifu haipendezi. Unajua sisi tunaokaa hapa mezani hatuchangii kama nyinyi, kazi yetu ni kuwapa nafasi  mseme, wakati mwingine zinatoka shutuma ambazo hatuna nafasi ya kubishana au kulumbana lakini wakati mwingine ni vizuri kutumia fursa hizi kusafisha baadhi ya mambo. Binadamu ni lazima uwe na staha ile ndogo tu kuwaheshimu binadamu wenzako," alisema Ndungai

Pamoja na hayo, Ndugai ameendelea kwa kusema "Katika bunge letu kinacholeta matatizo humu ndani ni tabia na lugha, tukirekebisha hayo mawili tutaenda vizuri tu lakini najua kundi hili ni kubwa hatuwezi kuwa wote tupo sawa, nitaendelea kulisemea lakini pale kwenye ulazima tutachukua hatua," alisisitiza Ndugai.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad