Ali Kiba: Simba Simuogopi Hata Kidogo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ali Kiba: Simba Simuogopi Hata Kidogo
Msanii Alikiba ambaye ni shabiki  wa klabu ya Yanga, amesema haiogopi wala kuihofia timu ya Simba hata kama wameanza vizuri kwa kugawa kichapo katika mechi za awali Ligi Kuu huku akidai mpira unadunda na muda wowote Simba itapotea.

Alikiba ameeleza hayo muda mchache alipomaliza mahojiano kwenye kipindi cha Planet Bongo kutoka East Africa Radio akiwa ameongozana na mtayarishaji wake wa wimbo mpya wa 'seduce me', Man Water ambao kwa sasa unazidi kuwa gumzo katika mtandao wa 'Youtube' kwa kufika watazamaji Milioni mbili.

"Simba hainitishi, Simba anafungiwa bandani ndiyo nimuogope mimi ?, kama kawapiga 7-0 Ruvu Shooting ni vijana wengine sisi hatuna shida japo ametufunga katika mechi ya watani wa jadi lakini hiyo ni kawaida na ndiyo maana ukisikia mpira unadunda maana yake ni kwamba mchezo unabadilika", alisema Alikiba.
Pamoja na hayo Alikiba aliweza pia kuzungumzia sakata la kuondoka kwa mchezaji ambaye alikuwa anampenda kwa umahiri wa kulisakata kabumbu  ambaye ni Haruna Niyonzima katika timu yao na kwenda Simba.

"Sidhani kwa kuondoka kwa mchezaji Haruna Ninyozima katika klabu yetu kama itaweza kutuletea madhara yoyote yale japo alikuwa ana kiwango kikubwa sana na ninamkubali, lakini ninaimani tumepata vyuma vingine vyenye nguvu kama vilivyoondoka ndiyo uzuri wa Yanga wana 'replace', ukibandua tu tunabandika japokuwa klabu imeingiza mpunga hatuna shida", alisema Alikiba.
"Ninachowaombea Yanga wakaze kwa kuwa naamini wana uwezo mkubwa sana na wachezaji wazuri sidhani kama kuna mapungufu yoyote yakawadhohofisha wachezaji au wana Yanga wakarudi nyuma. Sisi 'always' daima mbele hicho ndicho najua mimi", alisisitiza Alikiba.

Kwa upande mwingine, Alikiba amesema haoni hatari yoyote kwa klabu yake kutoa sare ya bao 1-1 na timu ya Lipuli FC mchezo uliyopigwa Agosti 26 mwaka huu katika mechi za ufunguzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kuwa bado Ligi haijanza kushika kasi huku akijipa matumaini kuwa timu yake itakuja kufanya maajabu katika mechi zijazo
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad