Korea Kaskazini Yaijaribu Japan

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Korea Kaskazini Yaijaribu Japan
Korea kaskazini imerusha makombora yake ambayo yalipita Japan kabla ya kudondokea baharini.
Makombora hayo yalisafiri kuelekea mashariki karibu kilomita elfu moja juu ya kisiwa cha Japan cha Hokkaido.

Tukio hilo limechochea tahadhari ya hatari ambayo watu walielekezwa kujificha katika maeneo yaliyo chini ya ardhi ama kwenye majengo yaliyo imara.
Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe amesema urushwaji huo wa makombora ambao haujawahi kutokea , umeleta kitisho kikubwa kwa taifa lake.Hakuna juhudi zilizofanywa na Japan kulitengua kombora hilo lakini ilitoa onyo la kiusalama ikiwaambia raia wake katika eneo la Hokkaido kujificha chini ya majumba yaliojengwa ardhini.

Wanajeshi wa Marekani na Japan wanafanya zoezi la pamoja katika eneo hilo la Hokkado, rais wa Korea Kusini Moon Jae-in aliagiza uwezo wa utumiaji wa nguvu ili kujibu shambulio hilo.
Ndege nne za Korea Kusini zilifanya zoezi la kurusha makombora siku ya Tuesday.
Bwana Abe alisema kuwa amezungumza na rais wa Marekani Donald Trump na kwamba wote wamekubaliana kuiongezea shinikizo Korea Kaskazini.

Katika mfululizo wa majaribio yake ya makombora ya hivi karibuni Korea kaskazini haijawahi kurusha makombora yaliyopita juu ya ardhi ya nchi hiyo, hivyo tukio hili la sasa limeleta wasiwasi mkubwa.

Katika siku za hivi karibuni Pyongyang ilijaribu kombora lake lililopata mafanikio kutokana na uwezo wake wa kuweza kuifikia Marekani na kuonyoa kuwa inasimamia mipango yake ya kushambulia kwa makombora eneo la Marekani la Guam, kilomita elfu mbiili kusini mashariki mwa Japan.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad