IGP Sirro: Jeshi la Polisi Aliwaonei Viongozi wa Vyama vya Upinzani Wala Halitumikii Siasa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

IGP Sirro: Jeshi la Polisi Aliwaonei Viongozi wa Vyama vya Upinzani  Wala Halitumikii Siasa
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Siro, amejibu tuhuma zinazotolewa na baadhi ya watu kuwa jeshi la polisi linatumika kisiasa na kuwaonea viongozi wa vyama vya upinzani, na kusema kuwa hakuna ukweli wowote juu juu ya hilo.

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Radio, IGP Sirro amesema jeshi la polisi halimkamati mtu kwa sababu ni kiongozi wa chama cha siasa au ni kiongozi wa dini, bali humkamata mtu iwapo kuna taarifa za uhalifu zilizowafikia kwani halifuati siasa., hivyo jukumu lao ni kuhakikisha usalama wa nchi.

“Polisi hakamati viongozi wa siasa, polisi hakamati viongozi wa dini, polisi anakamata mhalifu, na mhalifu anapomkamata anamhoji kama kuna ushahidi anampeleka mahakamani, kama hakuna ushahidi anamuachia”, alisema IGP Sirro.

IGP Sirro aliendelea kwa kuwataka wananchi wamuache afanye kazi yake kwani yeye ndiye anayewajibika na kusimamia amani, na kusema endapo utakamatwa na kukutwa hauna hatia, hawatasita kukuchia huru.

Msikilize hapa chini IGP Sirro, akielezea kwa undani suala la Jeshi la Polisi kutuhumiwa kutumika kisiasa.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad