Lwandamina Aula Yanga Aongezewa Mkataba

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Lwandamina Aula Yanga Aongezewa Mkataba
Kocha wa Yanga, George Lwandamina hana mpango wa kuondoka, maana tayari ameongezewa muda wa kuendelea kufanya kazi Jangwani.

Uongozi wa Yanga umeamua kumuongezea mkataba wa mwaka mmoja kocha wake George Lwandamina raia wa Zambia baada ya ule wa awali kumalizika Julai 16, mwaka huu.

Katika mkataba wake uliopita, Lwandamina aliiwezesha Yanga kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita na kuifikisha katika nusu fainali ya Kombe la FA kabla ya kutolewa na Mbao FC ya Mwanza.

Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa amesema  mchana kuwa, wameamua kumuongezea mkataba Lwandamina baada ya kuridhishwa na kazi yake.
“Tunaingia mkataba mwingine wa mwaka mmoja na Lwandamina kwani ule wa mwanzo umeisha na sasa kila kitu kipo tayari hivyo muda wowote tena kwa uwazi kabisa atasaini mkataba mpya.

“Tumejitahidi kwa uwezo wetu kuboresha mkataba wake mpya kwa kumuongezea maslahi kidogo ili apate motisha ya kufanya kazi yake ipasavyo,” alisema Mkwasa.
Lwandamina alitarajiwa kusaini mkataba huo muda wowote kuanzia jana mchana ili awe na uhakika wa kuendelea kufanya kazi yake kwa uhuru na kujiamini
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad