Manji Alivyomkataa Wakili wa Chadema Mbele ya Mahakama...Kisa Kizima Hichi Hapa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Diwani wa Mbagala kwa tiketi ya CCM, Yusuf Manji jana alisema mbele ya mahakama kuwa hataki kuwakilishwa na Wakili Peter Kibatala na kutaka abadilishe wakili kwa kile alichosema kuwa ni kutofautiana kwa itikadi za kisiasa.

Manji ambaye ni mmoja wa wafanyabiashara wakubwa nchini Tanzania aliiambia Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam jana kabla ya kuanza kusikilizwa kwa kwa maombi yake ya dhamana ambapo alishangaa yeye kama Diwani wa CCM kuwakilishwa na wakili ambaye ni mwanachama wa CHADEMA.

Manji anayekabiliwa na tuhuma za uhujumu uchumi, baada ya kumkataa wakili huyo aliwatambulisha mawakili wengine wapya wawili ambao watamuwakilisha.

Aidha, Mahakama Kuu jana ilitupilia mbali maombi ya dhamana ya Manji na kuanza mchakato wa kuipeleka kesi hiyo katika Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi na Rushwa baada ya Manji kukubali pingamizi la Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuomba kuyaondoa mahakamani maombi ya dhamana.

Mmoja wa mawakili wapya wanaomuwakilisha Manji, Alex Mgongolwa alisema walikubali kuondolewa kwa maombi hayo mahakamani hapo ili kupelekwa katika Mahakama ya Uhujumu Uchumi na Rushwa maarufu Mahakama ya Mafisadi  ambayo ndiyo yenye mamlaka ya kusikiliza maombi yao.

Manji anasota rumande kwa siku zaidi ya 30 sasa kutokana na kunyimwa dhamana kila anapofika mahakamani.


Toa Maoni Yako Hapa chini:
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad