Mkojo wa Wema Sepetu Watikisa Mahakamani Baada ya Kukutwa na Chembe Chembe za Bangi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

KESI inayomkabili staa wa Bongo Muvi, Wema Sepetu, jana ilichukua sura mpya baada ya mawakili wa pande mbili, ule wa utetezi na Jamhuri kuchuana kuhusu mkojo wa msanii huyo uliochukuliwa na kupimwa na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali wakati wa upelelezi wa polisi kuhusiana na mwanadada huyo kudaiwa kutumia madawa ya kulevya.

Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Thomas Simba, shahidi wa kwanza wa upande wa Jamhuri aliyefahamika kwa jina la Elias Mulima kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali akisoma ripoti ya uchunguzi alisema mahakamani hapo kuwa, mkojo wa Wema baada ya kupimwa ulikutwa na chembechembe za bangi.

Hata hivyo, wakili wa utetezi, Peter Kibatala, alisema ripoti hiyo iliyosomwa na Mulima ina upungufu mwingi wa kisheria. Baada ya kutokea malumbano hayo Hakimu Mkazi Simba aliwaomba mawakili wa pande zote mbili kuridhia apate muda wa kuipitia taarifa hiyo ya Ofisi ya Mkemia Mkuu ili itakapoendelea aweze kuitolea ufafanuzi. Awali, kesi hiyo iliahirishwa kusikilizwa kwa muda mahakamani hapo kutokana na wakili wa Wema kutokuwepo hivyo ikaanza kusikilizwa saa 6:30. Kesi hiyo iliahirishwa hadi Agosti 4, mwaka huu.

Katika kesi ya msingi, Wema anatuhumiwa kukutwa na msokoto mmoja wa bangi na vipande viwili vidogo vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08. Mbali na Wema washitakiwa wengine ni wafanyakazi wake wa ndani Angelina Msigwa (21) na Matrida Abbas (16), ambapo wote wanashtakiwa kwa kosa moja la kukutwa na kiasi hicho cha dawa za kulevya. Msanii huyo na wenzake hao wako nje kwa dhamana ya wadhamini wawili waliosaini Sh. 5,000,000 kila mmoja. Inadaiwa kuwa Wema na wenzake walitenda kosa hilo Februari 4, mwaka huu, nyumbani kwake Ununio, wilayani Kinondoni, Dar es Salaam.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. jamani bangi si ni sigara moshi vp apimwe mkojo ionekaniwe chembe chembe halafu isitoshe bangi mbona kitu cha kawaida tu hebu muacheni mtoto watu unless muna kisasi na yeye hee mbona vichekesho halfu wavuta bangi mbona wengi saba basi mukawashike wote munamuonea gere wivu tubna chuki binafsi muacheni mwana wa watu

    ReplyDelete

Top Post Ad