Ndugai: CUF ya Maalim Seif Hawatambuliki na Msajiri na Mimi Siwatambui

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ndugai: CUF ya Maalim Seif Hawatambuliki na Msajiri na Mimi Siwatambui
Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amefunguka na kusema hata yeye pia hawatambui CUF upande wa Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad kwa kuwa watu hao hawatambuliki kwa msajili wa vyama vya siasa nchini.

Spika wa bunge alisema haya siku alipokuwa anaongea na waandishi wa habari kuhusiana na mambo mbalimbali ya bunge na kusema hawezi kumtambua Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad kwa kuwa mtu huyo hatambuliki kwa msajili hivyo yeye ataendelea kumtambua Profesa Lipumba pamoja na Magdalena Hamis Sakaya kwa kuwa ndiyo watu wanaotambulika katika vyombo husika.

"Mimi sina tatizo lolote na chama cha siasa ila ni masuala ya utaratibu tu mwenye kumbukumbu ya vyama vya siasa na katiba za vyama vya siasa na viongozi halali wa vyama vya siasa ni msajili wa vyama vya siasa siyo mtu mwingine yoyote kwa hiyo linapotokea jambo la chama ambacho kina mvutano kazi yangu mimi ni kumuuliza huyo ambaye ndiyo muweka hazina wa vyama vya siasa ambaye ni msajili, akisema si mtambui na mimi nakuwa simtambui, akisema namfahamu basi na mimi nakuwa namfahamu lazima twende kwa utaratibu" alisisitiza Ngugai

Aidha Spika Job Ndugai alizisi kusema kuwa yeye hawezi kuibuka na kuanza kuwatambua watu ambao hawatambuliki kwa msajili wa vyama vya siasa nchini na kusema kwa kufanya hivyo atakuwa anakiuka utaratibu ambao upo na inaweza kuleta shida zaidi.

Msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi yeye anamtambua Mwenyekiti wa CUF taifa kuwa ni Profesa Ibrahim Lipumba na kumtambua Magdalena Hamis Sakaya kama Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad