Rais Magufuli Amgomea Mwekezaji Kusamehe Kodi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Rais John Magufuli amekataa ombi la kusamehe kodi kwa muda wa miaka 10 katika kiwanda cha saruji cha Kilimanjaro kilichopo jijini Tanga kwa kueleza kuwa kufanya hivyo ni kinyume na sheria.

Rais Magufuli ametoa msimamo huo wakati akitoa hotuba  katika hafla ya uzinduzi na  kujibu maombi yaliyokuwa katika risala ya kiwanda hicho, ambacho kilitaka kisamehewe kodi kwa muda wa miaka 10 kutokana na deni kubwa ambalo kinadaiwa katika taasisi za kifedha, zilizokopwa kama mtaji wa kukianzisha.

Sababu nyingine za kutaka kiwanda hicho kusamehewe kodi ni kutokana na mchango wake katika shughuli za kijamii ikiwemo kuchangia madawati na vyumba vya madarasa katika shule za jiji hilo pamoja na kusaidia huduma za maji.

Rais Magufuli amesisitiza kuwa serikali yake inahimiza viwanda ili iweze kupata mapato kupitia kodi, kwahiyo haiwezi kufanya uamuzi wa kusamehe kodi na kujikosesha mapato.

"Nianze kumshukuru rmwenye kiwanda kwa kutoa misaada kwa jamii, na kwa vile mifuko ya saruji 1300 aliyoitoa nilikuwa hapa nikija nitataka mnipeleke sehemu zilipotumika. Lakini uliniomba kusamehe kodi hilo ni ombi gumu. Kwa sababu wito wa serikali kuhimiza kujenga viwanda maana yake ni kwamba serikali ipate pesa tuweze kusomesha watoto bure, kuongeza madawa hospital nk. Ninachokuomba ni wewe tu ujipange ndiyo ushindani wenyewe.

Katika hatua nyingine, rais Magufuli ameupongeza uongozi wa kiwanda hicho kinachomilikiwa na wazawa kwa hatua hiyo ya kufanya uzalishaji na kutoa ajira kwa watanzania zaidi ya 100
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hongera Sana Baba. Viwanda na wawejezaji walipa kodi halali tunavitaka na tunawataka. Tax holiday imeshakufa. Ila tunaweza kuangalia vipi tunaweza kufanya friendly tax in certain privileges katika kuwapa masoko na order Aidi katika ujenzi WA DODOMA YETU. WALIPA KODI TUNAWAKARIBISHA NA SIYO WAKWEPA KODI. HAPA KAZI YU

    ReplyDelete
  2. Ndugu wawekezaji na wanaotaka kuwekeza kama Ashanti // GGM // BARRICK GOLD // na WAZAWA WOTW WENYE NIA NA LENGO LA UWEKEZAJI. NTAPENDA KUWASHAURI MKIFANYA IDEA DWVELOPMENT IN THE CORE OF YOUR INVESTMENT PLAN A TANZANIA SHOULD BE KEPT IN RHE CORE QUESTIOM HOW DO WE HELP THE COUNTRY'S DWVELOPMENT BY PAYING IT RIGHT. PALE HATUTOKUWA NA MATATIZO NA NYINYI NA TUNAWAKARIBISHA. LAKINI MKIANZISHA DILI HAPA MJUE TUTAGONGANA NA HAO WALAFI WENYE KUTAKA MASILAHI BINAFSI TUTAKUCHAMGAMYENI KIKAPU KIMOJA KAMA AKSIA. TUNATAKA WANFANYA BIASHARA NA WAWEKESAJI WAADILIFU AMBAO WATANUFAIKA NA KUTUNUFAISHA. IKIWEWE ULIPAJI KODI HALALI BILA UCHAKACHUAJI..HAPA KAZI TU

    ReplyDelete
  3. Ndugu wawekezaji na wanaotaka kuwekeza kama Ashanti // GGM // BARRICK GOLD // na WAZAWA WOTE WENYE NIA NA LENGO LA UWEKEZAJI. NTAPENDA KUWASHAURI MKIFANYA IDEA DEVELOPMENT IN THE CORE OF YOUR INVESTMENT PLAN A TANZANIAN SHOULD BE KEPT IN THE CORE QUESTIOM HOW DO WE HELP THE COUNTRY'S DEVELOPMENT BY PAYING IT RIGHT. PALE HATUTOKUWA NA MATATIZO NA NYINYI NA TUNAWAKARIBISHA. LAKINI MKIANZISHA DILI HAPA MJUE TUTAGONGANA. NA HAO WALAFI WENYE KUTAKA MASILAHI BINAFSI TUTAKUCHAMGANYENI KIKAPU KIMOJA KAMA AKSIA. TUNATAKA WAFANYA BIASHARA NA WAWEKEZAJI WAADILIFU AMBAO WATANUFAIKA NA KUTUNUFAISHA. IKIWEMO ULIPAJI KODI HALALI BILA UCHAKACHUAJI..HAPA KAZI TU

    ReplyDelete

Top Post Ad