Rais Magufuli Kuingilia Ugomvi wa Kanisa?

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Temeke limemuomba Rais Dkt John Pombe Magufuli kuingilia kumaliza mgogoro uliodumu kwa zaidi ya miaka 30 unaohusu umiliki wa kiwanja kilichopo Kitalu D Mtaa wa Everest jirani na Hospitali ya wilaya ya Temeke.

Mdhamini wa Kanisa la EAGT nchini Mchungaji Christom Isack Ngowi ametoa kauli hiyo kufuatia notisi inayowataka kuhamisha mali zote za kanisa kabla ya kesho Agosti 21, siku ambayo Manispaa ya Temeke imepanga kubomoa eneo hilo, kitendo ambacho waumini na viongozi wa kanisa hilo wamesema kingesubiri maamuzi ya barua waliyomuandikia Rais Magufuli kuhusu mgogoro huo.
Katika maelezo yao, viongozi na waumini wa kanisa hilo wameshangazwa na kile walichoeleza kuwa ni kutotekelezwa kwa maagizo ya mawaziri wa zamani wa ardhi akiwemo marehemu Mustafa Nyang'anyi na mwenzake Marcel Bujiku Komanya, ambao katika nyakati tofauti walizitaka mamlaka kulipatia kanisa la EAGT Temeke umiliki wa eneo hilo.

Kiwanja hicho kinagombewa kati yao na mfanyabiashara mmoja wa eneo hilo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Haya hayahitaji kumuingiza Mh Raisi. kuma ngazi na wizara husika na mmlliki halali kama anajulikana basi na apewe na si vinginevyo. Manispaa ya temeke na ikibidi kama kuna haja then MH LUKUVI Ni mchapa kazi na Muadilifu mzuri tu. MWACHENI MH RAISI JPM ATUFANYIE MAMBO MUHIMU ZAIDI YA MAENDELEO NA SIO KIWANJA..KUMRADHI MUANDIKAJI

    ReplyDelete

Top Post Ad