Sitegemei Mitandao ili Kuachia Nyimbo Zangu - Shilole

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





Sitegemei Mitandao ili Kuachia Nyimbo Zangu - Shilole
Msanii Zuwena Mohamed Shilole' amekanusha kauli yake ya kushindwa kuachia ngoma kwa kipindi cha miezi mitano kutokana na kudukuliwa kwa mtandao wake wa (Instagram) na badala yake alikuwa akiusoma mchezo huku akisubiria majibu ya ngoma 'Hatutoi Kiki.

Shilole amedai kuwa watu wanaozungumza kwamba yeye amekaa kimya muda mrefu ni kutokana na wengi wao kumiss kuona vituko na tashtiti zake katika mitandao ya kijamii hivyo hata wakati akiwa amejiandaa kutoa wimbo mpya bado alionekana kama kapooza.

"Siyo kweli kama nategemea Instagram kutoa kazi, kwani bila hiyo Insta zamani watu walikuwa wanafanyaje? Sijatoa wimbo kwa sababu nilitaka wimbo wa 'hatutoi kiki uendelee kusogea na siyo kwamba kwa sababu nilikuwa sina mtandao wa Instagram ndiyo nikaamua nitulie. Lakini kwa sababu najua kuna wasiosikiliza radio na na wasiotazama Tv ndiyo maana pia nilitulia kuusoma mchezo kwa kuwa nilitaka niwapate wote na mashabiki mashabiki wa mtandaoni ndiyo maana nilichelewa kidogo" Shishi alifunguka.

Hata hivyo Shilole ameongeza kuwa "mashabiki waliopokea wimbo wangu huu ndiyo mashabiki wa kweli siyo wale wanaosubiri tashititi za kukaa uchi au kelele zangu ila" Shilole.
Akizungumzia kuhusu mahusiano yake msanii Shilole amekanusha taarifa zinazoenea mitandaoni kuwa mume wake mtarajiwa ndiye mwanaume anayeonekana katika video yake mpya ya 'Kigori'.


----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad