Spika Ndugai Atoa ONYO Kwa Wabunge Watakaofanya Vurugu Bungeni

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Spika Ndugai  Atoa ONYO Kwa Wabunge Watakaofanya Vurugu Bungeni
Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema wabunge watakaofanya vitendo vya utovu wa nidhamu bungeni hawatavumiliwa na huenda adhabu ikaongezeka maradufu kwa wasiozingatia kanuni.

Ndugai aliyekuwa nje ya nchi kwa mwezi mmoja akitembelea Nigeria, Dubai na Iran alisema hayo jana alipojibu swali la mwandishi wa habari.

Spika Ndugai alisema vikao vya mkutano ujao wa Bunge vitaanza Septemba 5. “Tumekuwa tukiwatoa nje mara kadhaa lakini imefika mahali tumewafungia wengine mwaka mzima, ila sasa tumechoka wakirudi na wakaendelea na jeuri yao msishangae adhabu zikapanda na kuwa kubwa zaidi, kwa sababu tumechoka,” alisema.

Wabunge Halima Mdee (Kawe) na Ester Bulaya (Bunda Mjini), wote Chadema, walisimamishwa katika mkutano uliopita wa Bunge kuhudhuria vikao vya mkutano wa saba, nane na wa tisa hadi mwakani, ambapo watalipwa nusu mshahara na posho zinazoambatana nao kwa miezi 10 kwa mujibu wa kanuni ya 75 ya chombo hicho cha kutunga sheria
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hivi ndivyo omavyotakiwa hasa. posho ikipingua na njaa ilivyonuka. watanyyoka bila kuambiwa. mwaha Mlungu akutaze Ngwe. walamsaje wado kakaya. na Mkuluu .ale cho kuiona mwaha.sandenyi.

    ReplyDelete

Top Post Ad