Wakwe Wavunja Ndoa ya Mziwanda...Wamuozesha Nawal Kwa Mwanaume Mwingine Mwenye Pesa Bila Nuh Kutoa Talaka

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nuh Mziwanda ambaye hivi karibuni kumeibuka minong'ono kuwa ndoa yake imesambaratika, amefunguka kuhusu hilo na kukiri kuwa kweli ndoa hiyo imekufa bila talaka, huku mke wake akiwa mbioni kuolewa na mtu mwingine.

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Radio, Nuh Mziwanda amesema mke wake huyo hajampa talaka lakini ameolewa na mtu mwengine, huku vuguvugu kubwa lilianza kwa wakwe zake (wazazi wa mke wake)

Mimi na Nawal tulitengana tu, lakini baada ya hapo kumbe mwenzangu ameshaandaliwa mume wa kumuoa, mimi baada ya kugundua hilo nikaona bora nirudi kwenye dini yangu, kwa hiyo wazazi wa mke wangu walikuwa wanajua kuwa mtoto wao ananisaliti", alisema Nuh Mziwanda.

Nuh Mziwanda alipoulizwa kama alitoa talaka kwa mke wake huyo kama sheria ya ndoa inavyotaka watu wanapoachana, Nuh alisema hajatoa talaka na hawezi kutoa kwani tayari Nawal mke wa mtu.

"Mimi sijatoa talaka, na kufuatilia suala la talaka itakuwa kama najichoresha kwani wao wazazi wanajua kabisa kama ni mke wangu lakini wao wakaamua kumuozesha kwa mtu mwingine, kwa hiyo mimi naacha tu, mimi nitaangalia utaratibu wa kumlea mwanangu kwani bado mdogo hivyo bado yuko na mama yake", alisema Nuh Mziwanda.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. MAKUBWA!!! NDOA NYINGINE BILA TALAKA?? NDOA BATILI HIYO VITABU VYA DINI VINASEMA.

    ReplyDelete
  2. si ulifudia dini yako so ulikuwa unataka bi nawal afanye nini umwshampa jibu hapo btother usiji tete kwa njia yeyote ume kana ki plan kwa hivo wewe kivyako na yeye ndio hivo habari ya mjini kaolewa

    ReplyDelete

Top Post Ad