WASANII Acheni Uzembe – Mwanasheria Alberto Msando (+Video)

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwanasheria maarufu nchini Tanzania, Alberto Msando amefunguka kuwa Wasanii wa Tanzania huu ni muda wao muafaka wa kujitambua na kujithamini kwa kukaa siti ya mbele katika kushiriki kwenye vikao na mikutano inayojadili kwa upana masuala ya haki zao na sio kulalamika tu.

 Msando amesema hayo jana kwenye kikao maalumu kilichoitishwa na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kilichoongozwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Harrison Mwakyembe kwa lengo la kujadili namna ya kutatua changamoto za Wasanii.

“Wasanii lazima waache uzembe na kujisahau suala la kupigania haki zao suala la kuboresha kazi zao ni la kwao….Ni wakati wao hao kama wasanii kukaa siti ya mbele katika kupigania haki zao”,amesema Msando.

Hata hivyo Msando amewaasa Wasanii kushiriki vya kutosha kwenye mijadala na mikutano mbalimbali inayowahusu hao ili kuongeza uweledi katika kuboresha sanaa na kujua haki zao msingi.

♦Waziri Mwakyembe aunda Kamati ya kujadili namna ya kutatua changamoto za Wasanii (+Video)

Kitu cha kushangaza kwenye kikao hicho Wasanii ambao ndiyo wahusika wakuu mahudhurio yao yalikuwa mabovu ukilinganisha na Wadau na Waandishi wa Habari walioitikia wito huo.

 VIDEO:
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad