Wenger Awapa Wapinzani Habari ya Kutisha

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wenger Awapa Wapinzani Habari ya Kutisha
“Habari za sasa katika timu ni kwamba Laurent Kolcieny na Alexis Sanchez wote wamerejea” hayo ni maneno ya Arsene Wenger wakati huu kuelekea katika mchezo wao wa Epl mwishoni mwa wiki dhidi ya Liverpool.

Ujio wa Sanchez katika timu ya Arsenal imekuwa shangwe kwa mashabiki wao dunia nzima kwanza kwa kuwa wanamuhitaji sana na pili wanaamini kwamba wameishinda vita iliyokuwa ikiwakabili ya kumbakisha Alexis.

Kama unakumbuka jina la Sanchez lilitawala sana katika msimu wa usajili akihusishwa na timu mbalimbali huku mkataba wake ukiwa umebakiza mwaka kuisha lakini sasa Sanchez anaonekana anabaki Gunners.

Arsenal walimkosa Sanchez katika michezo yao iliyopita ya Premier League na hii ilionekana kuwaoa shida sana kutokana na Mchile huyu kuwa mwamba wa Arsenal tangu msimu uliopita.

Kurejea kwa Alexis Sanchez kunaleta kitu kipya ndani ya kikosi cha Gunners ambapo sasa Alexandre Lacazette ambaye ameanza vizuri msimu anaenda kuongezewa nguvu mpya kwa kucheza na Sanchez kikosini.

Sanchez anaonekana kupania sana kurudi Arsenal kwani Wenger amesema “sio rahisi kumzuia, hajacheza muda mrefu na anaonekana ana hamu sana kurudi uwanjani, mechi ni Jumapili na tutaona nini tunaweza kufanya”

Kuhusu kuondoka kwa Sanchez Wenger amesema “ni mchezaji mkubwa na mzuri na nataka abaki na sisi na aangalie jinsi ya kuendelea kuwa na sisi, nina uhakika hasumbuliwi na tetesi kwani ameshazoea”

Arsenal watasafiri kuelekea Anfield siku ya Jumapili kuikabili Liverpool katika mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza huku wakiwa na kumbukumbu kwamba mara ya mwisho kushinda Anfield ilikuwa mwaka 2012.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad