Yusuf Manji Apinga Mkojo Wake Kukutwa na Madawa ya Kulevya.....

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

KESI inayomkabili mfanyabiashara Yusuf Manji ya kutuhumiwa na matumizi ya dawa za kulevya leo Ijumaa, Agosti 22, 2017 imeanza kutolewa ushahidi wa vipimo vilivyochunguzwa kwa mkemia mkuu wa serikali na majibu yake huku wakili wake akipinga kielelzo hicho cha mkojo hakikuwa halali.

Ushahidi huo umeanza kusikilizwa mbele ya Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha kwa nyakati tofauti shahidi wa kwanza alikuwa Ofisa Mkuu wa Makosa ya Jinai na Naibu Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum Dar es Salaam, Ramadhan Kindai na Askari Polisi Kitengo cha Upelelezi cha Makosa ya Jinai, Christopher.


Wakifafanua mahakamani hapo wameeleza hatua zote walizozifuata tangu Manji aliporipoti Kituo Kikuu cha Polisi, Februari 9 mwaka huu na kupelekwa kwa mkemia kwa ajili ya kuchukuliwa vipimo vya mkojo na hatimaye kugundulika anatumia madawa ya kulevya.

Kwa upande wa utetezi, Wakili wa Manji, Hoodson Ndusiepo aliukataa ushahidi wa barua iliyoandikwa ya Manji kupelekwa kwa Mkemia Mkuu ili kuchukuliwa vipimo vya mkojo kwa madai kuwa barua hiyo ilitakiwa kuwa na sahihi ya mteja wake kuridhia akachukuliwe vipimo hivyo.

 Pia wakili huyo alimhoji shahidi wa kwanza juu ya hati ya mashtaka iliyofunguliwa dhidi ya Manji inayoonesha mteja wake anatuhumiwa kwa matumizi ya dawa za kulevya aina ya Heroine na kwa nini inatofautiana na vipimo vya mkemia vinavyoonyesha aina ya madawa yaliyogundulika wakati wa vipimo kuwa aina ya Benzodiazepine.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. wanamuonea wanakisasi na yeye jamani tuogopeni mungu serekali ya uonevu simameni na haki wanotumia madawa ya kulevya mbn wako wamejaa na hawakamtwi kina ray c nendeni soba kama kweli muntafuta muwawwke rumande wote

    ReplyDelete
    Replies
    1. Unamaanisha hatumii hayo madawa au?

      Delete
    2. Mwisho wa maovu ni aibu ulimuona akityumia

      Delete

Top Post Ad