Zaidi ya Marais 20 Kutoka Mataifa ya Afrika Kushuhudia Kuapishwa kwa Kagame Leo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Zaidi ya Marais 20 Kutoka Mataifa ya Afrika Kushuhudia Kuapishwa kwa Kagame Leo
Rais wa Rwanda Paul Kagame anaapishwa leo kuiongoza nchi hiyo kwa muhula wa tatu wa miaka 7
Hii ni baada ya kushinda uchaguzi wiki mbili zilizopita kwa kupata asilimia 98 ya kura.
Sherehe za kula kiapo zinafanyika kwenye uwanja wa taifa Amahoro mjini Kigali.
zaidi ya marais 20 kutoka mataifa ya Afrika wanahudhuria sherehe hizo.
Miongoni mwao ni rais wa Sudan Omar Al Bashir ambaye anasakwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC.

Rwanda siyo mwanachama wa mahakama hiyo.
Katika uchaguzi wagombeaji wengine 2 Philippe Mpayimana na Frank Habineza wa chama cha Green waliambulia asilimia 1 jumla ya kura zao.

Uchaguzi huo ulikosolewa na baadhi ya mataifa kama Marekani ambayo ilisema hali ya siasa nchini Rwanda inatoa fursa tu kwa mtu mmoja pekee kwendelea kuiongoza nchi hiyo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad