BAVICHA Kula Sahani Moja na Wasiojulikana

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

BAVICHA Kula Sahani Moja na Wasiojulikana
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA) wameahidi kushughulika na watu wanaodaiwa wasiojulikana wanaotekeleza matukio ya uhalifu yakiwepo ya uuaji, utekaji, na uchomaji moto ofisi za wanasheria.

Akizungumza na Wanahabari leo kwenye makao makuu ya Chama , Kinondoni jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa BAVICHA, Patrobas Katambi amesesema hayo huku akiwataka viongozi wa vijana nchini kuandaa utaratibu wa kuwashughulikia watu hao wasiojulikana.
Aidha. Katambi amesema kuwa vijana wanapaswa kuchukulia jambo la Lissu kupigwa risasi kwa uzito ikiwa ni pamoja na kuonyesha kuchukizwa na mattukio ya kihalifu yaliyowahi kufanywa huko nyuma na watu wanaotajwa kuwa 'wasiojulikana' na kama watashindwa basi atajiuzurru wadhifa wake.

"Natoa agizo kwa viongozi wote wa vijana hapa nchini kuratibu utaratibu mzuri wa chinichini namna ya kuwashughulika hawa wahalifu ambao hawajulikana. Inawezekana hawa watu wasiojulikana wananguvu kuliko vyombo vya dola. Naomba niseme tutawashughulikia kwa namna isiyojulika, kwasababu wao ni watu wasiojulikana. Nitajiudhuru nafasi yangu endapo hili litashindikana.
Pamoja na hayo Bw. Katambi ameongeza kwamba viongozi wa kisiasa wanapaswa kukutana kwa ajili ya majadiliano ya ya matukio yanayotokea kwani hali ya hatari haipo kwa CHADEMA tu bali kwa viongozi wote huku akitolea mfano tukio la viongozi wa CUF walipovamiwa wakiwa kwenye mikutano.

"Napendekeza viongozi wa kisiasa waweze kukutana kwa ajili ya majadiliano ya namna gani ya kukabiliana na hawa watu wasiojulikana wakadhibitiwa. Mfano Alphonce Mawazo, aliyeuawa na watu wasiojulikana, lakini Ben Saanane naye amepotezwa na watu wasiojulikana na hata viongozi wa CUF walivamiwa mkutanoni na watu wasiojulikana. Ni vyema jambo hili mlizingatie sana.


----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Katambi Aliyekupa Airtime amekosea.
    Kimantiki wewe huna haki ya hayo unayoyasema.
    na cha zaidi ni mwelekeo wa Uhamasishaji usio na msingi wala mashiko ..
    Kama umeshindwa Ajira... Jiuzulu uangalie ustaarabu mwingine ..eleza mlikijua nini na nani alipewa majukumu gani kwa maagizo ya nani.. na atekeleze episode ipi in series.. mwingine. TUNAKUJA
    Juu ya hisia za bawicha kujua msijihami.. Upelelezi unaendelea na mtajie

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tanzania tunawatu wasijiliwa wengi mfano hapo juu , nyerere alipanga kuua elimu iliatawale milele sasa matokeo ndio hayo miaka 100 ccm maendeleo hakuna lakini wapo wanaotetea halafu anarudi nyumbani hakuna umeme

      Delete

Top Post Ad