Zitto Kabwe Ataka Uchunguzi wa Kimataifa Kuchunguza Shambulio Alilofanyiwa Tundu Lissu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Zitto Kabwe Ataka Uchunguzi wa Kimataifa Kuchunguza Shambulio Alilofanyiwa Tundu Lissu
Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema unahitajika uchunguzi wa kimataifa dhidi ya shambulio la Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.

Akituma ujumbe wake kwenye Twitter, Zitto amesema kwamba vyombo vya ndani  vinaweza visiaminike kutokana na uzito wa tukio hilo.

Amesema kwamba ‘’Washambuliaji wa Lissu wamelenga kutunyamazisha. Iwapo tutaendelea kunyamaza, watashinda. Hatuwezi kuwapa nafasi hiyo, tunaongea kuhusu haki,”amesema.

Lissu alishambuliwa Alhamisi wiki hii wakati alipokuwa akifika nyumbani kwake mjini Dodoma akitokea katika vikao vya Bunge.


----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. KAMA NDUNGAI ALITOA WAZO LA NUSU POSHO YA SIKU.
    BASI UJUE ZITO HACHUKUI POSHO.
    KWA HIYO HAKUMLAZIMU .
    UCHUNGUZI HUU NI WAZO LAKE ZITO AJILI YA AJALI ZINAZO TOKE PIA ZINAWASIBU ..UONGO ZITO

    ReplyDelete
  2. Hapa ndipo ninapomuona Zito Kabwe kuwa ni mtu wa hovyo. Akili yake yote imegubikwa na upumbavu wa kuamini yakuwa mataifa ya nje hasa yale ya kizungu na serikali zake ni matakatifu katika masuala ya uhalifu. Marekani na serikali yake kwa mfano imehusika na mambo mengi ya uvunjifu wa haki za binadamu nje na ndani ya taifa hilo. Mfano utumwa kwa watu wa weusi. Utumiaji wa silaha za kinyuklia kule japani,uvamizi wake wa kijeshi kule iraq bila ya idhini ya umoja wa mataifa. Miaka nenda rudi matukio kadhaa ya utata yanayohusiana na upotevu wa maisha ya watu yakiendelea ndani ya Marekani lakini hakuna mpuuzi mwanasiasa wa upinzani wa Marekani atakaekubali au kushauri wachunguzi wa mataifa ya nje kuja kufanya uchunguzi ndani ya ardhi yao na huo ndio uzalendo wa kweli. Wamerekani licha ya mapungufu yao lakini katika suala la uzalendo kwa taifa lao wametukuka haswa . Vipi kukimbilia wachunguzi wa mataifa ya nje bila ya kushauri kuundwa tume huru ya ndani ya kitanzania kuchunguza suala hili? Tumeona jinsi tume zilizoundwa za kitanzania na watanzania kufuatilia masuala ya madini zilivyofanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu kabisa mpaka wazungu jasho linawatoka. Nitajie nchi gani safi kuja kuchunguza mambo yetu ya ndani? Uingereza hivi karibuni watu wameungua moto na kupoteza maisha yao katika ajali ambayo hakika kama ingetokea Tanzania watu wangeimba nyimbo za wachunguzi wa kimataifa. Ni upuuzi na akili tegemezi za baadhi ya viongozi wa kiafrika wanaomini sisi waafrika hatuwezi kujisimamia wenyewe kwa lolote lile na ni ujinga tulioujenga waafrica kuwakabidhi wakoloni uhuru wetu wa akili waendelee kututawala miaka nenda miaka rudi huku wakituacha masikini wa hali na mali. Zito ni miongoni mwa wanasiasa wapumbavu wasiojiamini na kutamani nchi za kigeni kuendelea kututawala.

    ReplyDelete

Top Post Ad