Chid Benz: Madee ni Mbea na Mnafki

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Chid Benz: Madee ni Mbea na Mnafki
Rapa Chid Benz ambaye kwa sasa amekuwa gumzo katika kila kona ya mitandao ya kijamii baada ya yeye kusema ana kolabo na 2pac, amefunguka kwa kumtolea povu Madee na kumwambia yeye ni mbea ndiyo maana haishi kumnanga kila kukicha.

Chid Benz ameeleza hayo kupitia kipindi cha 'Friday Night Live' (FNL), kinachorushwa na EATV pamoja na EA Radio baada ya siku kadhaa kupita tokea alipofanyiwa 'interview' na eNewz na kudai ana kolabo na 2pac, jambo ambalo watu wengi waliamini msanii huyo ameanza kuharibikiwa akili kutokana na dawa za kulevya na kupelekea Madee kutoa maoni yake binafsi kwa kudai ni bora yeye ambaye havuti hata sigara.

"Unaweza ukawa huvuti hata sigara lakini ukawa mbea, kwa sababu Madee watu tumnajua kama ni mbea na mnafki maana anapenda kuninanga, anahisi labda mimi ipo siku nitafanya kitu", alisema Chid Benz.
Pamoja na hayo Chid Benz aliendelea kwa kusema "mtu kama anaku-post kitu katika mitandao ya kijamii halafu chini yake anakuandikia 'ndiyo maana mimi sivuti hata sigara' 'that means' anaonyeshea watu kwamba kuna kitu Chid Benz anatumia au anavuta ndiyo maana yeye hatumii sigara kwa hiyo mimi amenitengenezea ubaya mpaka kupelekea watu ku-comment kwamba madawa yamenisababisha nichanganikiwe", alisisitiza Chid Benz



----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad