IGP Sirro Awatembelea Askari Ambao Nyumba Zao Zimeteketea Kwa Moto

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

IGP Sirro Awatembelea Askari Ambao Nyumba Zao Zimeteketea Kwa Moto
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amewasili eneo la nyumba za polisi zilizoteketekea kwa moto.

Nyumba hizo zilizopo Kata ya Sekei ziliteketea kwa moto jana Jumatano usiku.

IGP Sirro amesema Rais John Magufuli ametoa Sh260 milioni kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za kuishi askari hao.

Amesema Jeshi la Polisi kupitia bajeti yake limetoa Sh40 milioni kwa ajili ya ujenzi huo.

IGP Sirro amesema jeshi hilo pia litatoa Sh1 milioni kwa kila familia iliyoathiriwa na moto huo. Katika nyumba zilizoteketea familia 14 zilikuwa zikiishi.

Kiongozi huyo wa Jeshi la Polisi amesema Rais Magufuli ameagiza Wakala wa Majengo (TBA) kutoa jengo la kuwahifadhi askari hao wakati ujenzi wa nyumba ukifanyika.

Amewataka wananchi wenye nia njema kuzisaidia kwa chochote walichonacho familia za waliounguliwa mali zao.

IGP Sirro na ujumbe wake ameelekea Tengeru kukagua jengo la TBA watakalotumia kwa muda askari hao.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad