Maalim Seif Asimulia Maendeleo ya Afya ya Tundu Lissu Baada ya Kumtembelea Nairobi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Maalim Seif Asimulia Maendeleo ya Afya  ya Tundu Lissu Baada ya Kumtembelea Nairobi
Katibu  Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, ameeleza maendeleo ya afya ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), baada ya kumtembelea hospitalini Nairobi, Kenya.

Akihojiwa na Redio ya Idhaa ya Kiswahili Deutsche Welle (DW) ya Ujerumani jana, Maalim Seif alisema Lissu anaendelea vizuri na hajapoteza mwelekeo.

“Jana (juzi) nilimtembelea Lissu na nilipata moyo sana, kwa kweli anaendelea vizuri ukizingatia mtu ambaye alipigwa risasi zaidi ya 30, anapata nafuu haraka haraka.

“Bado hajapoteza mwelekeo akili yake ipo timamu, ametuhakikishia haya yaliyotokea hayatamrudisha nyuma katika kuwatetea wanyonge.

“Anazungumza vizuri, yuko makini sana anajua anachokisema na mimi nimepata moyo jinsi nilivyomuona,” alisema Maalim Seif.

Alisema kutokana na mambo yanayoendelea nchini, lazima kuwapo na mjadala wa  taifa   kuona tumekosea wapi na kujirekebisha.

“Mambo kama haya kutokea Tanzania ni jambo ambalo kila Mtanzania lazima aingiwe na wasiwasi kwa sababu hakuna hata mmoja na hasa mwanasiasa ambaye ana usalama wa maisha yake.

“Kama taifa tuzungumze kuona tumekosea wapi na kujirekebisha,” alisema.

Kuhusu uchunguzi wa tukio hilo, alisema hata kama vyombo vya dola vya ndani vitafanya  si aibu kwa nchi kutafuta msaada kwa wengine.

“Yako mambo mengine yaliyotokea huko nyuma na bado hatujaaambiwa yalikwenda vipi, tunaambiwa tu uchunguzi unaendelea. Ni vizuri wananchi waone matokeo ya uchunguzi huo…si aibu kwa nchi kutafuta msaada kwa wengine,” alisema.

Lissu alipigwa risasi  zinazokadiriwa kufikia 32, Septemba 7, mwaka huu, alipokuwa akirejea nyumbani kwake Area D mjini Dodoma baada ya kutoka kuhudhuria kikao cha Bunge na kujeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za mwili wake.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad