Jambazi Sugu Aliyeongoza Mauaji Auwawa na Polisi Dar

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Jambazi Sugu Aliyeongoza Mauaji Auwawa na Polisi Dar
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, jana Septemba 12, maeneo ya Kivule Chanika lilifanikiwa kumuua jambazi sugu aitwae Anae Rashid Kapela aliyekuwa akitafutwa na jeshi hilo kwa muda mrefu akituhumiwa kushiriki matukio mbalimbali ya ujambazi likiwemo la mauaji ya polisi wanane wilayani Kibiti.

Hayo yamesemwa leo na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Mambosasa alipokuwa akizungumza na wanahabari jijini Dar.

“Baada ya kupewa taarifa na wasamalia wema, Jeshi hilo lilifika na kuizingira nyumba alimokuwa lakini alifanikiwa kutoka na kutaka akitoroka. Polisi walipomsimamisha alikimbia ndipo wakampiga risasi ya goti na kuanguka.

“Alipohojiwa aliwataja wenzake pamoja na matukio makubwa ya uhalifu aliyoshiriki kuyafanya likiwemo hilo la kuwaua Askari Polisi wanane na kupora silaha zao kisha kukimbia,” alisema Mambosasa.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad