Kauli ya IGP Sirro Yamchanganya Msigwa Aamua Kumpa Neno Hili

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kauli ya IGP Sirro Yamchanganya Msigwa Aamua Kumpa Neno Hili
Mbunge wa Iringa Mjini (CHADEMA) Mchugaji Peter Msigwa amefunguka na kuonyesha kutoridhishwa na kauli ya  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Nyakoro Sirro kusema Tundu Lissu hakuwahi kutoa taarifa juu ya watu wanaomfuatilia.

Mbunge Msingwa ambaye sasa yupo nchini Kenya kwenye matibabu ya Tundu Lissu ameonyesha kusikitiswa na taarifa hiyo ya IGP ambayo aliitoa Septemba 8, 2017 katika mkutano wa waandishi wa habari na kusema kiongozi huyo hakuwahi kutoa taarifa yoyote polisi juu ya gari ambalo lilikuwa likimfuatilia kabla ya kupatwa na shambulizi hilo la kupigwa risasi.
"Kamanda Sirro Ulitaka Lissu atoe taarifa gani zaidi? Sisi wengine ni wanasiasa, hatuna mafunzo ya kijeshi, Polisi wala Kikachero. Silaha yetu kubwa ni kipaza sauti (microphone), kazi yetu ni kupaza sauti , hoja inapaswa kujibiwa kwa hoja! Siyo kwa mabomu ya machozi, sio kwa virungu na bunduki. Inaonyesha jeshi letu la polisi uwezo wake mkubwa ni kupambana na vyama vya siasa hasa CHADEMA na CUF kuwalinda wakuu wa wilaya na mikoa" aliandika Mchungaji Msigwa
Aidha Msigwa anasema anaumia kuona Tundu Lissu akiteseka kwa ajili ya kutetea haki na Demokrasia ya taifa la Tanzania na kusema alichofanyiwa Tundu Lissu kinampa ujasiri wa kusonga mbele.
"Mungu anakataza kumwaga damu isiyo na hatia! machozi yanitoka kuona rafiki yangu Tundu Lissu akiteseka kwa kutetea  haki na demokrasia ya taifa letu, amewakosea nini? Inanipa ujasiri wa kusonga mbele, sitanyamaza, tunakupenda Lissu wewe ndiye shujaa wetu" aliandika Msigwa


----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Msigwa , Mbona unajichanganya na kutaka kuwachanganya wasomaji wako .
    Mpaka leo hii hujui tofauti ya kujisemesha kwa kiki za mitandao
    na kwenda uka kaa foleni mpaka wakati wako unafika unajieleza baada ya kutoa kitambulisho na kuhakikiwa.
    halafu unafungua Ripoti na unapewa namba ya kumbukumku toka kwetu ili baada ya kulifanyia kazi tunawasiliana na wewe.
    Amka chungaji.
    na kama ndio hivi basi unawatia hofu wapiga kula wako. juu ya uelewa wako. Huwezi Kumuuliza IGP wetu swali la kipumbavu tena Bado Mitaondaoni au Unatafuta Kiki kama Wale...???

    ReplyDelete

Top Post Ad