Maafisa Utumishi Watakaochelewesha Mishahara Kukiona

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Maafisa Utumish Watakaochelewesha Mishahara Kukiona
Serikali imetangaza kiama kwa maofisa utumishi wote ambao watachelewesha mishahara kwa watumishi bila sababu za msingi.

Aidha, katika uwajibikaji huo, Wakurugenzi wa halmashauri za wilaya na manispaa watakuwa wakifungiwa mishahara yao kama itabainika katika maeneo yao kuna watumishi wanacheleweshewa mishahara.

Onyo hilo limetolewa leo bungeni na Waziri wa nchi ofisi ya Rais Utumishi na Utawala bora Angela Kairuki wakati akijibu swali la nyongeza na Innocent Bashungwa (Karagwe-CCM).

Mbunge huyo alitaka kujua serikali inawaambia nini watumishi ambao wamekuwa na uzembe katika kubadilisha mishahara ya watumishi ambao wanastahili na wakati mwingine kuchelewesha mishahara hiyo.

"Katika hili hatutakuwa na huruma na mtumishi yeyote kama tulivyofanya kwa baadhi ya maofisa na ndivyo tutakavyofanya na tumeamua kwenda mbali zaidi kwa kupanga kufungia mishahara wakurugenzi ambako maeneo yao kutokea mkanganyiko huo," amesema Kairuki

Kuhusu malimbikizo ya watumishi wanaodai kwa ajili ya nauli nyakati za likizo, amesema kiasi cha Sh 1  tririoni zimetengwa kwa ajili ya kuwalipa watumishi hao baada ya kukamilisha kuhakiki madai yao.


----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad