Mtatiro: Msajili Anataka Kubadili Sheria ili Awe na Mamlaka Ndani ya Vyama Lengo Kuua Upinzani na Kuweka Mamluki

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Nimeiona Barua kutoka kwa Msajili wa Vyama vya Siasa kuvitaka Vyama vya siasa vitoe maoni kuhusu utungwaji wa Sheria Mpya ya Vyama vya Siasa. Nilijua kwamba jambo hili lingefuata. Serikali inachukua hatua hii wakati huu ili kubariki "UJINGA" wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa siku za usoni.

Lengo kubwa kuliko yote ni kuweka kipengele kitakachoeleza kuwa "Msajili wa Vyama vya Siasa anaweza kuingilia mambo ya ndani ya vyama vya siasa na kwamba uamuzi wake utakuwa wa mwisho."

Yaani, kumlinda mtu mmoja, LIPUMBA, ili aimalize CUF, kunafanya hadi sheria zibadilishwe haraka ili AIBU zinazofanywa na Msajili zilindwe.

Tumewahi kuwaeleza huko nyuma mara kadhaa, kwamba Mahakama Kuu imewahi kutamka bayana katika maamuzi mbalimbali, kuwa "Msajili wa Vyama vya Siasa hana mamlaka ya kuingilia maamuzi ya vikao vya vyama vya siasa kwa njia yoyote ile."

CUF ilipoanza kupigwa vita na LIPUMBA akiwa mtumiwaji mkuu, wapo watu walitucheka. Tuliwaambia shambulio dhidi ya CUF ni shambulio dhidi ya demokrasia.

Tusubiri wapitishe hiyo sheria yao, uone vyama vitakavyoporwa uhuru wa ndani. Na huko ndiko CCM inapenda twende, maana yanyewe haiwezi kuguswa na Msajili ambaye obvious anateuliwa na Mwenyekiti wa CCM.

#NOTE; Hata ikitungwa sheria hii hivi sasa, mashauri ya CUF yaliyoko mahakamani yatatumia viwango vya mamlaka ya msajili yaliyotajwa kwenye Sheria Namba 5 ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992 (sheria ya sasa).

#Kama mngekuwa na akili mngetunga sheria ya kuhimiza ujenzi wa kiwanda kimoja kikubwa kila kata. Lakini mko likizo!

Mtatiro J
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mtatiro Welkome beki. Nasikia ulikwenda wewe Na plofesa huko Malekani kuchukua luzuku.
    Ngapi mmeingia nazo?
    Nasikia Plofesa kakuachia zote wewe. Kweli?

    ReplyDelete

Top Post Ad