Polisi Kula Sahani Moja na Wanaofanya Vitendo vya Uhalifu wa Makosa ya Mitandaoni

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Polisi Kula Sahani Moja na Wanaofanya Vitendo vya Uhalifu wa Makosa ya  Mitandaoni
Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Barnabas Mwakalukwa amewataka wananchi kwa ujumla wanaofanyiwa vitendo vya uhalifu mitandaoni wasiende TCRA bali wanapaswa kutoa taarifa katika jeshi la polisi.

ACP Mwakalukwa amebainisha hayo wakati alipokuwa anazungumza katika mkutano wa pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuhusu suala zima la uhalifu wa makosa ya mitandao ambapo kwa sasa limeshika kasi kubwa

"Chochote kinachofanyika ambacho ni kosa jinai nawaomba msiende Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kwa watoa huduma wa mitandao ya simu mbalimbali wala katika vyombo vya kutolea habari bali unapaswa uje katika kituo cha polisi utoe taarifa zako kama ni kosa la jinai kwa sababu mkienda huko uchunguzi utakuwa shida kwa maana wewe mwenyewe utaweza kusababisha hata yule aliyekutendea uhalifu atoroke", amesema ACP Mwakalukwa

Pamoja na hayo, ACP Mwakalukwa ameendelea kwa kusema "Kutokana na kukua kwa teknolojia vitu vingi vimekuwa vikifanyika 'online' kwa hiyo hii mitandao ya kijamii imeonekana ni muhimu sana kwenye maendeleo, lakini pia imebadilisha mbinu ya kufanya uhalifu katika mitandao ya kijamii kwa kutumiwa na baadhi ya watu kutapeli, hata kutishia kuua, hivyo jeshi la polisi limejipanga kwa ajili ya kushughulikia makosa ambayo yanatokana na mtandao", amesema Mwakalukwa.

Kwa upande wake,Kaimu Mkurugenzi wa TCRA, Thadayo Ringo amesema analishukuru jeshi la polisi kwa kuweza kuwasaidia katika kuwatatulia changamoto mbalimbali hasa za kiusalama huku akiwataka wananchi watakaopata matatizo katika mtandao kwenda kutoa taarifa polisi ili waweze kuwasaidia kabla ya kufika kwao.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. huu ujumbe ni viongozi wote waserikali na vikosi vya Polisi, jinsi hali inavyoendelea Tanzania inamuelekeo nchi kwenda kwenye udiktata, msipo angalia mtaanzisha machafuko kwenye nchi. SOMALIA, Wanazungumza luga moja asilimia 98 dini moja, walianzaje machafuko mpaka leo ? kila kitu mnakataza nyinyi wazima au tusemaje, wapumbavu wajinga wasenge au vipi.

    ReplyDelete

Top Post Ad