Raia Wawili wa China Wafukuzwa Nchini

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Raia Wawili wa China Wafukuzwa Nchini
Uongozi wa mkoa wa Morogoro umewakamata raia wawili kutoka nchini China na kuwaamuru kurejea kwao baada ya kukaidi mara kadha amri zilizokuwa zikiwataka kusimamisha shughuli walizokuwa wakizifanya kinyume cha sheria katika kiwanda wanachokimiliki cha Marumaru cha Zhong Fenq kilichpo katika kijiji cha Maseyu.

Hatua hiyo inakuja baada ya Waziri mkuu kutoa agizo kutokana na malalamiko ya Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, Omary Mgumba kuwa wawekezaji hao kutoka China wanaendesha shughuli za uchimbaji bila ya kuwa na kibali.

Ambapo Mgumba alieleza kuwa tangu mwaka 2010 wawekezaji hao wameendesha shughuli zao bila kulipa kodi za Serikali na tozo za halmashauri, hivyo kuikosesha Serikali mapato.

Mbunge huyo ambaye machimbo hayo yako jimboni kwake, alisema licha ya uongozi wa mkoa kwenda eneo hilo na kuizuia kampuni kuendelea na uchimbaji hadi itakapopata vibali ilikaidi na kuendelea na shughuli zake kama kawaida.

Majaliwa alisema iwapo wahusika watabainika kuwa hawajafuata sheria, kanuni na utaratibu hatua zichukuliwe dhidi yao ikiwa ni pamoja na kuwaondoa katika eneo hilo chini ya ulinzi na kuwasiliana na ubalozi wa China nchini.

Hatimae, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt Stephen Kebwe alitoa agizo kwa vyombo vya ulinzi kuwakamata raia hao na kuamuru warudishwe nchini kwao baada ya kugundulika wanafanya kazi bila kufuata utaratibu,sheria, na kanuni za nchi.


----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad