Rais Kenyatta Aijia Juu Mahakama kwa Kubatilisha chaguzi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Rais Kenyatta Aijia Juu Mahakama kwa Kubatilisha chaguzi
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amelitaja jopo la majaji wa mahakama ya juu liliobatilisha uchaguzi wake wa urais kuwa 'Wakora'

Awali alikua ametaka kuwepo na utulivu na kusema kuwa ataheshimu uamuzi wa mahakama lakini baadaye akaonyesha msimamo tofauti katika mkutano wa hadhara.
Mahakama hiyo ilisema kuwa uchaguzi wa mwezi uliopita ulikumbwa na udanganyifu na kuagiza kufanyika kwa uchaguzi mwengine katika kipindi cha siku 60.
Uchaguzi huo uliokuwa umezua wasiwasi wa kutokea kwa ghasia za baada ya uchaguzi kama zile zilizotokea 2007.

Ijapokuwa ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi uliopita hazikufikia kiwango cha 2007, ghasia za siku kadhaa zilisababisha vifo vya watu 28.
Tume ya uchaguzi nchini Kenya ilikuwa imemtanfaza rais Kenyatta kuwa mshindi kwa kiasia cha kura milioni 14 lakni matokeo hayo yakapigwa mahakamani na mpinzani wake mkuu Raila Odinga.

Katika hotuba aliyotoa katika runinga, rais Uhuru kenyatta alisema kuwa ni muhimu kuheshimu sheria hata iwapo unatofautiana na uamuzi wa mahakama ya juu.Alitaka kuwepo kwa utulivu akisema: Jirani yako ataendelea kuwa jirani yako licha ya lololote litakalotokea.
Ujumbe wangu muhimu leo ni Amani. Lakini alikuwa na msimamo mwengine wakati alipohutubia mkutano wa hadhara katika soko moja jijini Nairobi.
Raila Odinga akifurahia uamuzi wa mahakama uliofutilia mbali uchaguzi wa rais Uhuru Kenyatta  

Raila Odinga akifurahia uamuzi wa mahakama uliofutilia mbali uchaguzi wa rais Uhuru Kenyatta
Aliwatyaja jaji Maraga na majaji wenzake kua wakora, akisema aliamua kubatilisha uchaguzi wake.
Aliomuonya jaji Maraga kwamba baada ya uchagyzi huo kufutiliwa mbali bado yeye ndio rais na sio tena rais mteule kama ilivyokuwa.

Munanielewa? Maraga anafaa kujua kwamba hivi sasa anakabiliana na raius aliye mamlakani , alisema bwana Kenyatta mwenye umri wa miaka 55.
Tunawaangalia kwa karibu.Lakini wacha tumalize uchaguzi mwanzo,Hatuogopi.
Kufuatia uchaguzi huo waangalizi wa kimataifa kutoka muungano wa Ulaya , ule wa Afrika pamoja na wale wa Marekani walikuwa walisema kuwa hakuna udanganyifu uliofanyika na kumtaka Odinga kukubali kushindwa.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad