Waziri wa Ujenzi Atoa Agizo kwa Balaza la Ujenzi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Waziri wa Ujenzi Atoa Agizo kwa Balaza la Ujenzi
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa ameliagiza baraza la ujenzi nchini kuhakikisha linaandaa taarifa kamili kuhusuiana na ujenzi ili kuondoa changamoto mbalimbali zinazojitokeza mara kwa mara pindi miradi inapotaka kuanza.

Prof. Mbarawa amesema hayo leo katika kikao chake na baraza la ujenzi, ambapo kimewakutanisha wataalamu wa ujenzi kutoka ndani na nje ya nchi kwa lengo la kuangalia changamoto zilizopo kwenye sekta hiyo na kuzitafutia ufumbuzi.

"Kwa sasa hakuna taarifa sahihi kuhusu masuala ya ujenzi nchini, sekta ambayo inachangia kwa asilimia 14 ya pato la taifa na haikui kiushindani na nchi zilizoendelea kwa kiwango cha kisasa", amesema Prof. Mbarawa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Ujenzi nchini, Prof. Mayunga Mkunya amesema hakuna ushirikiano mzuri katika sekta ya ujenzi hali ambayo inachangia kukosa kuwa na mipango endelevu.




-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad