Winga wa Azamu Joseph Kimwaga Nje ya Dimba kwa Miezi Minne

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Winga wa Azamu Joseph Kimwaga  Nje ya Dimba kwa Miezi Minne
WINGA wa Azam FC, Joseph Kimwaga, anatarajia kukaa nje ya dimba kwa muda miezi minne baada ya kubainika ya kuwa amechanika mtulinga wa kati ‘meniscus’ kwenye goti lake la mguu wa kushoto.

Kimwaga hivi sasa yupo nchini Afrika Kusini tokea Ijumaa iliyopita akifanyiwa matibabu ya goti lake hilo, aliloumia wakati Azam FC ikijiandaa na mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Ndanda ulioisha kwa matajiri hao kushinda bao 1-0 wiki mbili zilizopita.

Kwa mujibu wa Daktari wa Azam FC, Mwanandi Mwankemwa, aliyeambatana na Kimwaga nchini humo, ameuambia mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz kuwa mchezaji huyo alifanyiwa vipimo jana Jumatatu na Dr. Nickolas kwenye Hospitali ya Vincent Palloti iliyopo jijini Cape Town nchini humo.

“Jumatatu (4/9/2017)alifanyiwa vipimo na kuthibitika amechanika Meniscus upande wa kati (meniscus mfano wake tunautoa kwa mafundi anapofunga nati anaweka washa kwanza halafu ndio anakaza nati juu yake Mwenyezi Mungu amemuaamba kila binadamu na hiyo washa inayoitwa meniscus, ipo katikati ya goti kuimarisha goti, ipo upande wa kati na pembeni. Hebu gusa sikio lako pembeni, meniscus inafananishwa au kulinganishwa na kuta za sikio lako).
“Vile ameumia mtulinga wa kati ACL(Anterior Cruciate Ligament),” alisema kwenye ripoti aliyoipokea kutoka kwa Dr. Nickolas.

Mwankemwa alisema baada ya kufanyiwa kipimo hicho, Kimwaga anatarajiwa kulazwa kesho Jumatano saa 9.00 Alasiri, huku akitarajiwa kufanyiwa upasuaji mdogo (athroscopy) siku inayofuata Alhamisi kabla ya kutoka hospitalini Septemba 9 mwaka huu na kurejea nchini siku nne baadaye (Septemba 13) saa 12.00 jioni kwenye Uwanja wa Mwl Julius Nyerere (JNIA).

Upasuaji wa kwa njia ya Athroscopy ni ule wa kisasa kabisa ambao wataalamu hutumia vifaa maalum, ambavyo huingizwa kwenye goti ambavyo hufanya matibabu na kuondoa matatizo yote katika eneo hilo, faida yake humfanya mchezaji kurejea mapema uwanjani kuliko ule wa kupasuliwa goti zima.

Winga huyo mara baada ya kufanyiwa upasuaji Alhamisi anatarajiwa kukaa nje ya dimba kwa kipindi cha miezi minne kutoka siku ya upasuaji.
Azam FC tunamtakia kila kheri Kimwaga katika matibabu yake hayo, yaweze kwenda salama kama yalivyopanga na hatimaye aweze kurejea dimbani mapema.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad