Askofu Amfananisha Magufuli na Mugabe kwa Uwajibikaji Wake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Askofu Amfananisha Magufuli na Mugabe kwa Uwajibikaji Wake
Askofu wa Jimbo Katoliki Zanzibar Agustino Shao, amefananisha Rais Magufuli na Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, kwa uwajibikaji na kukemea vitendo vya rushwa.

Kwenye taarifa iliyotolewa na Ikulu kwa vyombo vya habari, imeeleza kuwa Askofu Shao ameyasema hayo kwenye ibada ambayo ilihudhuriwa na Rais Magufuli visiwani Zanzibar kwenye kanisa la Mtakatifu Joseph, na kusema kwamba Rais Mugabe alichukua hatua za kupigania maslahi ya Wazimbabwe na sasa hivi wananeemeka na matunda hayo, kitendo ambacho amedai Rais Magufuli anakifanya kwa sasa, na kuwataka watanzania kumuunga mkono.
"Hatutaweza kusema tunaimaliza rushwa wakati tunaendelea kuishi kwa kupata fedha ambazo hatujazifanyia kazi. Ni lazima tuishi machungu ya kuimaliza rushwa. Ni lazima tuishi machungu ya kuweka uadilifu katika utendaji wetu, tusipoishi maisha hayo tutaishi dunia mbili, dunia ya rushwa na dunia ya kujenga uchumi na uadilifu wa watanzania, " amesema Askofu Shao.
katika salamu zake akimshukuru Askofu SHao kwa mahubiri mazuri, amewahakikishia Watanzania kuwa serikali itachukua hatua kupambana na rushwa kulinda rasilimali za nchi, na kuwataka Watanzania wote kuungana katika hilo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad