Bomomoa Bomoa Kuhamia Kwenye Makanisa, Misikiti Kimara Kesho

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Bomomoa Bomoa Kuhamia Kwenye Makanisa, Misikiti Kimara Kesho
Nyumba za ibada 24 zinatarajiwa kubomolewa kesho  na Wakala wa Barabara Nchini (Tanroads)  ili kupisha upanuzi wa barabara ya Morogoro inayoanzia Kimara hadi Kiluvya.

Ubomoaji wa nyumba hizo za ibada ni mwendelezo wa uboamoaji wa nyumba takribani 1300 za wakazi wa maeneo hayo zinazodaiwa kujengwa ndani ya mita 121.5 ya barabara hiyo.

Nyumba zaidi ya 1000 zimebomolewa mpaka sasa hali inayosababisha baadhi ya wananchi kulala nje kutokana na kukosa makazi .

Akizungumza na gazeti la Mwananchi leo kwa njia ya simu Mhandisi wa Tanroads Kimara ambaye  anasimamia

ubomoaji huo ,Jonson Rutechula amesema kesho watakuwa na kazi maalum ya kubomoa nyumba za ibada tu.

“Tumewaambia viongozi wa misikiti na makanisa, waondoe vitu kesho  tunakuja kubomoa.Tutabomoa makanisa 14 na misikiti 10 kuanzia eneo la Kimara hadi Kiluvya”amesema

Amesema  shughuli ya ubomoaji wa nyumba imekamilika kwa asilimia kubwa ,zimesalia  nyumba za ibada tu.”Kama unavyoona karibu ubomoaji wa nyumba za makazi  umekamilika tulibakiza  nyumba za ibada”amesema

Ameongeza kwamba  “Kesho  tutabomoa makanisa 14 na misikiti 10 kuanzia eneo la Kimara hadi Kiluvya na tutaanza kazi hiyo asubuhi”amesema Rutechula.

Hata hivyo mwandishi wetu alitembelea Kanisa la Mtakatifu Maria Parokia ya Kimara  na kukuta baadhi ya waumini wakitoa  vyombo nje na walipoulizwa baadhi ya viongozi waliokuwepo kanisani hapo walikataa kuzungumza .

“Sisi siyo wasemaji, kama unataka habari njoo kesho na kamera zako uchukue  matukio lakini pia mtafute Paroko yeye atakwambia nini kinaendelea maana sisi si wasemaji”amesema  mmoja wa waumini hao
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad