Nape Awataka Watanzania Waache Ushamba

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mbunge wa Mtama, kwa tiketi ya (CCM) Nape Moses Nnauye amefunguka na kuwataka watu kuacha ushamba kwani kusifu au kukosoa juu ya jambo fulani ni kazi ambazo Mungu amewapa watu kuzifanya hivyo mtu baki hupaswi kukerwa na kuhangaika na hayo.

Nape Nnauye amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter na kusema mtu ambaye anachukizwa na watu ambao wana sifu juu ya jambo fulani au kukosoa basi huyo mtu ni mshamba.

"Mungu kagawanya kazi, wengine kusifu, wengine kukosoa, wengine yote pamoja! Kwanini unakerwa na kuhangaika na mgawanyo wa kazi? !Acha ushamba" alisistiza Nape Nnauye

Aidha kiongozi huyo amezidi kusisitiza kuwa watu wanapaswa kutimiza wajibu wao na kuacha kuhangaika na watu ambao wanasifia juu ya mambo au kukosoa.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mwambie Zito Nape. Yeye kila kiti kwake Ni kosoa beza.
    Tena Si Mshamba Tu.
    Labda neno nzuri au jina litakuea HAYAEANI kwa muono wangu.
    Sasa ameajiriwa Na aksia Kama msemaji mjiteua. Au sijui kateuliwa siku Ile pale MORENA.
    UNAZO HABARI HUKU TWITA.
    NASIKIA YY NI JIRANI FESI BUKU.

    ReplyDelete
  2. Hivi USHAMBA maana yake nini vile?

    ReplyDelete
  3. Kiasi fulani nashindwa kumuelewa ndugu yangu Nape. Mtu alishakuwa mpaka waziri wa nchi tena wa habari alafu anafungua kinywa chake hadharani kuwakashifu washamba kwa maana ya watu wanaoishi mashambani au vijijini ni wajinga hawajitambui. Neno ushamba linatokana na mtu aneishi au aliekulia kijijini na kutokuwa na uweledi na mambo ya mji lakini sioni sababu atolewe mfano wakuwa ni mtu mpumavu Nape inabidi achunge ulimi wake na ajue anachokizungumza wananchi wanakichukulia kimezungumzwa na Kiongozi la sivyo akija kuvamiwa na watu wasiojikana asijekasema kaonewa. Watanzania wengi wanaishi mashamba neno linalotumika zaidi Zanzibar kwa maana ya vijijini. Kwa hivyo Nape anaona watu wanaishi mashamba ni washamba ni watu wa hovyo give me a break . Mtu akisifu na anachokisifu kikastahili kusifiwa basi hakuna shida. Lakini mtu akiusifia upumbavu lazima watu watakereka na ni haki yao ya msingi kabisa kutoa maoni yao wewe Nape usijaribu kuwashurutisha watu jinsi ya kusema. Vile vile mtu akikosoa na anachokikosoa kinastahili kukosolewa basi hakuna shida lakini mtu akikosoa kisicho stahili kukosolewa basi lazima ajibiwe na asahihishwe kwa nguvu zote. Kwa Mfanao tuliona baadhi ya wapumbavu fulani walivyokuwa wakimvaa Maghufuli kwa kumkosoa kwa kejeli wakati anapigania Makinikia ya dhahabu. Watanzania wengi tilijua waliokuwa wanamkosoa Muheshimiwa raisi walikuwa wanakosea na kwa bahati nzuri watu hawakukaa kimya walijibu kwa kusahihisha yakuwa Magufuli yupo right na wanaomkosoa hawaitakii mema nchi yetu na mwisho wa siku imekuja kuthibitika yakwamba Maghuful yupo sahihi. Kwa hivyo Nape shut up nenda kawahubirie wananchi wako wa mtama nadhani wanahitaji maendeleo kuliko maneno ya vijembe mitandaoni.

    ReplyDelete

Top Post Ad