Ni Wakati Hivi Vikundi vya Maombi Vipigwe Marufuku- Alberto Msando

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ni Wakati Hivi Vikundi vya Maombi Vipigwe Marufuku- Alberto Msando
Wakili Maarufu Alberto Msando amefunguka na kusema kuwa anatamani baadhi ya vikundi vinavyoanzishwa kwa ajili ya maombi vipigwe marufuku kwani watu waonzisha vikundi hivyo wanalenga kujitafutia pesa na huku wananchi wa hali ya chini wakizidi kuumia.

Msando amesema hayo kupitia mtandao wake wa Instagram baada ya Nabii mmoja nchini Tanzania kuuandaa ibada ya maombi ya kuvunja laana ya kutembea kwa miguu huku akiwaahidi watu wote watakaofika kwenye misa hiyo watapata baraka na kupata magari na kusema magari yao yameshikiliwa na shetani baharini.
"Na kuna watu wataenda. Kuna watu wataamini masuala ya imani ni magumu sana ila kadri siku zinavyozidi kwenda haya mambo yanaongezeka. Hali ngumu ya maisha inasababisha baadhi ya watu kuamini kila kitu. Na wanaoanzisha hivi vikundi vya maombi wanafaidika sana. Ni wakati baadhi ya vikundi vipigwe marufuku" alisisitiza Msando
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kazi zitokazo kwa Mungu zitaishi na hakuna wa kuzuia. Lakini zile zisizo zake hazitaishi na zitayeyuka kama barafu jangwani. Si vyema kutumia maoni binafsi kwaajili ya kuzuwia kazi za mungu kwani upumbavu wa Mungu ni zaidi ya hekima ya mwanadamu. Unapoona mambo usiyoyaelewa iombee jamii yako na umwambie Mungu atupe macho ya kuona uso wake na kutambua hila za shetani badala ya hekima za shetani

    ReplyDelete
  2. Pointless,mwanasheria anachosema ni true Tena zaidi ya Mia kwa mia, kwa sasa watu maisha yakiwachanganya wanajiita eti ni watumishi wa mungu, mungu hajaajiri mtu kire mtu anao uwezi wa kuwasiriana na mungu wake site wana wa mungu we are at the same level, waache utaperi wafanye kazi, hapa Kaz tu

    ReplyDelete

Top Post Ad