Raila Odinga Abadirisha Mawazo Ataka Mazungumzo na Rais Kenyatta

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Raila Odinga Abadirisha Mawazo Ataka Mazungumzo na Rais Kenyatta
Kiongozi wa muungano wa upinzani (Nasa) Raila Odinga ‘amebadili gia angani’ na sasa anasema yuko tayari kwa mazumgumzo na Rais Uhuru Kenyatta, katika msingi uchaguzi uwe huru na wa haki na siyo kuunda serikali ya muungano.

Odinga ametoa msimamo huo wakati akitangaza kusitishwa kwa maandamano ya kuipinga Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC).

Amesema badala yake, Nasa watafanya mikutano ya hadhara kuanzia Jumatano ili kuwaeleza wafuasi wao kwa nini uchaguzi mpya wa rais usifanyike Oktoba 26 kama ilivyopangwa na IEBC.

Alisema timu yake iko tayari kwa mazungumzo "hata ingekuwa jana" muradi tu kikao kiwe ni namna gani uchaguzi huru na wa kuaminika unaweza kufanyika kulingana na amri ya Mahakama ya Juu na wala si juu ya kuunda serikali ya muungano.

“Hisia ambazo zimejengeka ni kwamba mimi ndiye ninayetaka serikali ya nusu mkate,” alisema.

Kauli hiyo ilikuwa ya kurejea madai ya uongozi wa Jubile kwamba maandamano ya Nasa yalikuwa njama zilizolenga kuhakikisha kwamba Odinga na wenzake wanajumuishwa katika serikali ya muungano kama inavyokuwa baada ya vurugu zilizoibuka katika uchaguzi wa mwaka 2007/2008.

“Kamwe sijawahi kumwita Kenyatta na kutaka serikali ya muungano. Madai hayo, kwa hiyo ni ya upuuzi.”

“Ikiwa uchaguzi ni huru, haki na wa kuaminika, niko tayari wakati wowote. Nasa inataka kuunda serikali. Tunataka mkate kamili kwa sababu tulishinda. Tulishinda uchaguzi wa Agosti 8,”alisema akiwa katika Uwanja wa Ndege wa Wilson mjini Nairobi.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad