Sheria ya Vyama vya Siasa Kufuta Mikutano ya Hadhara ya Vyama vya Siasa Hadi Wakati wa Uchaguzi Pekee

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Sheria ya Vyaamaa vya Siasa Kufuta Mikutano ya Hadhara ya Vyama vya Siasa Hadi Wakati wa Uchaguzi Pekee
RASIMU ya Sheria ya Vyama vya Siasa inayotarajiwa kufanyiwa marekebisho kabla ya Uchaguzi Mkuu ujao, inapendekeza kufutwa kwa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa hadi wakati wa uchaguzi pekee.

Rasimu hiyo, ambayo imetumwa kwa vyama vya siasa kwa ajili ya kutoa maoni yao, pia inapendekeza ruzuku ilipwe mara moja na kwa vyama vyote kulingana na idadi ya kura za urais katika Uchaguzi Mkuu.

Iwapo mabadiliko hayo yatapelekwa bungeni, uwezekano wa kupitishwa kuwa sheria ni mkubwa kutokana na idadi kubwa ya wabunge kutoka chama tawala (CCM) kinachoongoza Serikali ambayo itawasilisha muswada wa mabadiliko hayo.

Rasimu hiyo imekuja wakati vyama vya upinzani vikipigia kelele kutoheshimiwa kwa Katiba na sheria na kuminywa kwa demokrasia iliyofanya vishindwe kupiga siasa kwa uhuru, hasa baada ya Serikali kupiga marufuku mikutano ya hadhara na maandamano.
Serikali imeruhusu mikutano ya ndani ambayo pia imesababisha viongozi kadhaa kukamatwa au kuhojiwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kupanga mikakati ya uchochezi.

Na tayari vyama vya upinzani vimeshaingiwa na hofu dhidi ya mapendekezo hayo, vikisema yanalenga kufuta sheria ya mwaka 1992, kwa mujibu wa viongozi waliozungumza na Mwananchi jana na juzi.

Katika Rasimu ya Muswada wa Mabadiliko ya Sheria hiyo, Kifungu cha 45(2) kinaeleza kuwa mikutano ya vyama haitaruhusiwa katika kipindi ambacho hakuna uchaguzi, isipokuwa itakayoitishwa na wabunge, wawakilishi na madiwani katika maeneo yao.
Kuhusu ruzuku, rasimu ya muswada huo katika Kifungu cha 59 (1) inaeleza itatolewa mara moja katika mwaka wa fedha na waziri atazingatia hali ya kiuchumi na kifedha katika wakati husika.
“Sheria inayotungwa kwa kuangalia mtu au kundi la watu ni sheria mbaya,” alisema mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia alipoulizwa maoni yake kuhusu mapendekezo hayo.
“Kinachofanyika sasa kinaturudisha miaka 25 nyuma. Uhuru alioupigania Mwalimu (Julius)Nyerere upo wapi? Uhuru wa kukusanyika, uhuru wa mawazo?”
Mbatia, ambaye pia ni mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) alisema nchi inaendeshwa kwa matukio na kushauri kuwa maendeleo ya nchi ni lazima yawe shirikishi.
“Ajenda ya Malengo ya Milenia ya amani, haki na uimara wa taasisi unatoweka nchini,” alisema Mbatia, ambaye ni mbunge wa Vunjo.
“Zamani, mataifa ya nje yalikuwa yanakuja kujifunza siasa hapa kwetu, lakini kwa hali inavyoendelea sasa, watakuja kujifunza kitu gani? Tunapaswa kurejea katika mchakato wa Katiba ya Jaji Warioba, Katiba imara itatuondoa hapa tulipo na kwenda mbele zaidi.”
Serikali ilitangaza kupiga marufuku mikutano ya hadhara mwaka 2016, ikisema inataka watu wajikite kufanya kazi za maendeleo na kwamba yataruhusiwa mwaka 2020 wakati wa Uchaguzi Mkuu.
Tamko hilo kwanza lilitolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, lakini alipoulizwa bungeni alisema ilihusu jimbo lake na baadaye likatolewa na Jeshi la Polisi wakati Chadema ilipotangaza mikutano ya hadhara ya kuishtaki Serikali, kabla ya Rais John Magufuli kuweka bayana wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma za polisi Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Kwa wakati wote, vyama vya upinzani vimekuwa vikipinga marufuku hiyo kwa maelezo kuwa inapingana na Ibara ya 20 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano inayotoa uhuru kwa watu kukusanyika na kuitishana kwa lengo la kujadili, kufanya mkutano au kupeleka ujumbe kwa jamii au Serikali kuhusu jambo lolote ilimradi wanafanya hivyo kwa amani.

“(Muswada huu) Umehalalisha makatazo ambayo hayakuwa kwa mujibu wa sheria na hasa tamko la kuzuia mikutano ya vyama vya siasa sasa yanawekwa kwenye sheria,” alisema mkurugenzi wa itifaki, mawasiliano na mambo ya nje wa Chadema, John Mrema.
“Kama chama tutakaa kupitia kifungu kwa kifungu na kutoa msimamo kuhusu rasimu ya muswada huu.

“Muswada huu umeweka vifungu vingi ambavyo siasa sasa imefanywa kuwa kosa la jinai.”
Pamoja na vyama vya siasa, hasa vya upinzani kupinga mapendekezo hayo, Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi ameyatetea kuwa yametoka kwa wadau.

Akizungumza na Mwananchi juzi, Jaji Mutungi alisema mapendekezo yaliyomo kwenye rasimu hiyo yametoka kwa wadau, akisema ndio waliowezesha kupatikana kwa rasimu hiyo.
“Yeyote mwenye hoja afike ofisini kwangu,” alisema Jaji Mutungi.

Katika Kifungu cha 47 cha mapendekezo hayo, vyama vya siasa vinazuiwa kuajiri, kusambaza, kuunda vikundi vya ulinzi au kuwa na muundo sawa na wa Jeshi la Polisi au chombo chochote cha ulinzi na usalama cha Serikali.
Pia, vyama vinazuiwa kuratibu au kutoa mafunzo ya kijeshi na kutumia silaha.
Mapendekezo hayo pia yanalenga kuondoa utaratibu uliopo sasa wa vyama vya siasa kuwa na wanachama wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu kutokana na kifungu cha 32 kuzuia vyama kufanya shughuli za kisiasa kwenye maeneo ya kazi, shule au vyuo na majengo ya Serikali.
Mapendekezo hayo yanapendekeza adhabu ya Sh3 milioni au kifungo cha miezi sita jela au adhabu zote kwa pamoja kwa yeyote atakayekiuka kifungu hicho.

Mapendekezo hayo pia yanabadilisha utaratibu wa kuwasilisha ilani za uchaguzi. Kifungu cha 31(1)(c) kinapendekeza vyama kupeleka ilani hizo kwa Msajili wa Vyama vya Siasa badala ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Mrema, ambaye aliratibu kampeni za urais cha Chadema mwaka 2015, alisema mapendekezo hayo yanampa mamlaka makubwa Msajili kama ya kimahakama kwa kuwa anaweza kuagiza kupelekewa taarifa yoyote ya chama cha siasa, jambo alilosema ni la hatari.

Alikuwa akirejea Kifungu cha 36 cha rasimu hiyo kinachopendekeza kuwa kama chama cha siasa kitaitwa au kualikwa katika mafunzo ndani au nje ya nchi, ni lazima kitoe taarifa kwa Msajili siku saba kabla na kikikiuka kitakumbana na faini ya kati ya Sh1 milioni hadi Sh10 milioni au kifungo cha miezi sita gerezani au vyote kwa pamoja.
Sheria wanazotaka wao
Wakizungumza kuhusu rasimu hiyo, viongozi wa kisiasa walilaumu kuwa inalenga kuwabana.
“Tangu nchi hii ilipopata uhuru Desemba 9, 1961, sheria zinazotungwa ni zile wanazotaka wao na ndiyo maana zimekuwa na matatizo,” alisema mwenyekiti wa chama cha United Peoples’ Democratic (UPDP), Fahmi Dovutwa.

“Wao wamepanga na wanataka wanachotaka wao. Mimi nimepeleka mapendekezo, lakini sidhani kama yatafanyiwa kazi. Wanachokifanya si sawa. Huwezi kuweka sheria ngumu, huwezi kutubana tusifanye siasa.

“Sawa tutawasikiliza kwa kuwa wametaka wao. CCM wanaogopa kivuli chao na itakuja kuwagharimu siku moja. CCM isifikirie itapata kila siku na upinzani utakosa kila siku. Ipo siku CCM watang’oka na itawagharimu.”

Maoni kama hayo alikuwa nayo mwenyekiti wa Chama cha Kijamii (CCK), Costantine Akitanda ambaye alisema mapendekezo hayo yana lengo la kumaliza siasa na watu kama yeye wanaweza kujiondoa kutoka katika siasa.

“Sitaki kuamini kama kuna wabunge wanaojitambua hata wa CCM ambao watakubali kupitisha mapendekezo hayo,” alisema Akitanda. “Kwa nini tunashughulika na kuweka sheria kandamizi zinazokinzana na Katiba? Tunapaswa kutengeneza sheria zinazotekelezeka. Mimi nitakuwa miongoni mwa watakaoachana na siasa kwa sheria hizi na itafika wakati mzazi akimsikia mwanae anataka kuwa mwanasiasa atamzuia kwa sheria za aina hii.

“Ngoja tusubiri tukiitwa kuijadili na hata ikienda tutaitwa Kamati ya Bunge na tutaipinga.”
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Itakuwa safi tu kama huo mswaada wa kusitiswa mikutano yahadhara utapelekwa bungeni kwani jitihada zinatakiwa kuchukuliwa kuwahamisisha watanzania hasa vijana kutambua thamani ya muda au wakati. Wakati ukipita haurudi tena kunabakia majuto. Watanzania wanatakiwa kuhamasishwa kutumia muda wao kufanya kazi kwa bidii badala ya kupoteza muda wao kuwasikiliza wanasiasa hasa wa upinzani kwenye mikutano ya hadhara na ahadi zao hewa. Wakati wa uzembe wa akili kwa mtanzania kudanganywa na wanasiasa kwa manufaa yao binafsi umekwisha. Tanzania ina mwalimu mmoja tu wa kweli wa maisha na watanzania wakimsikiliza basi wametoka kimaisha. Na mwalimu huyo si mwengine bali muheshimiwa raisi Maghuful. Maghuful Siku zote huwa hadanganyi huwa anazungumza ukweli na kuwaeleza hali halisi watanzania bila hofu hata kama baadhi ya watu wanakwadhika na ukweli. Anaposema sileti chakula cha bure watu wafanye kazi walime wajitume baadhi ya watu wanalaani lakini ukweli laana hizo zitawarejea wenyewe kwani nnaimani hata Mungu anafurahia anaposikia kiongozi wa watu akisema ukweli na kuhimiza watu kufanya kazi. Maghuful ni mpango mzima kwa matatizo ya watanzania kwani hakuna dawa yenye ladha tamu ya kutibu maradhi sugu dawa yenye unafuu kwa uchungu ni kudungwa sindano.

    ReplyDelete

Top Post Ad